Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » JACK PATRICK AFIKISHWA POLISI KWA KUMPIGA CHUPA ZA USO "MREMBO HAFSA"

JACK PATRICK AFIKISHWA POLISI KWA KUMPIGA CHUPA ZA USO "MREMBO HAFSA"

tangazo

STAA wa Bongo anayetesa kwenye mitindo, Jacqueline Patrick anakabiliwa na msala wa kumtwanga na chupa nusu kumuua mrembo anayejulikana kwa jina la Hafsa Sasya

 Habari zilizopenyezwa na chanzo chetu kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, ishu ilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi ya Januari 26, mwaka huu ndani ya Ukumbi  wa Elements Lounge uliopo Masaki, Dar.


 Jack alifikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay  na  kufunguliwa kesi yenye jalada namba  OB/RB/1678/13  KUJERUHI.


KAULI  ZAO :

KAULI YA JACK
“Ni kweli kulitokea ugomvi siku ile...na ni kweli nilihojiwa na Polisi wa Kituo cha Oysterbay, lakini nimetoka kwa dhamana na kesi imekwenda mahakamani.”

 
KAULI YA HAFSA
“Mimi na Jack tulikuwa marafiki lakini nashangaa amenipiga na chupa bila sababu. Nimeshonwa nyuzi tatu. Siku ile alinikuta nimesimama na rafiki yangu mara akanipiga kikumbo kisha akaenda chooni, aliporudi akanikumba tena, nilipomuuliza ikawa kosa; akanipiga na chupa.


“Imeniuma sana maana amenipa jeraha usoni mwangu bila sababu ya msingi, maana sina ugomvi naye. Kwa sababu hili suala lipo mikononi mwa sheria, naamini itachukua mkondo wake.”
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger