tangazo
Mwakilishi wa Tanzania wa mwaka jana katika shindano la Big Brother Africa Julio amesema TID anaweza kuwa mwakilishi mzuri kwenye shindano hilo mwaka huu.
Julio alisema hayo jana wakati alipokuwa akitambulisha ngoma aliyoshirikishwa na Lucci, Waters Up kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM na ndipo alipoulizwa nani anafaa kushiriki katika shindano hilo mwaka huu.
“TID anafaa sana katika mashindano ya Big brother kwasababu ni mcheshi pia ni mtu mwenye sifa zote za kushiriki shindano hilo la Big Brother, ” alisema Julio.