"UGOMVI WA MSICHANA" WASABABISHA BUIBUI AGONGWE NA PIKIPIKI NA KUTEGUKA MIGUU YOTE
tangazo

Msanii wa Bongo Flava Frank Kitende aka Buibui amelazwa katika
hospitali ya taifa ya Muhimbili baada ya weekend hii kugongwa na
pikipiki na kupelekea kuvunjika mguu wake wa kushoto na wa kulia
kuteguka.
Akiongea na 255 ya Clouds FM Buibui amesema tukio hilo limetoa usiku
alipokuwa ametoka kufanya video ya wimbo wake na msichana aitwaye Lina J
aliyeamua kumsindikiza baada usiku kuwa mnene.
Akiongea na 255 ya Clouds FM, Buibui amesema:
“Yule msichana nikamwambia kama vipi huu muda umeenda sana, mida ya
saa saba saa nane, turudi tu home tukapumzike kwasababu kesho tena
tunamalizia hii video,huku na huku tukaondoka, lakini katika wale vijana
tuliokuwanao, mmoja simfahamu ila mwingine namfahamu, sasa huyo mshkaji
alikua anamtaka huyo msichana, mi sijawahi kumtongoza, kwasababu
namchukulia kama dada yangu naye ananichukulia kama kaka yake , na mimi
sikupenda kwasababu yule sio malaya, nikaona bora nimrudishe yeye kwanza
halafu na mi ndio nirudi kulala Kinondoni.
Buibui akiwa Muhimbili
Kumshusha yule, sasa yule jamaa alikuwa kakaa mbele akawa kama
amemaindi hivi, ‘kwanini Buibui kakubali tumrudishe huyu kwanza,
kwanini asituache naye’, kwasababu alikuwa anafosi wanishushe mi kwanza
halafu wao waendelee nae safari yao. Sasa yule dada akaniambia “Buibui,
nipeleke mimi kwanza huwezi jua naweza nikafanyiwa kitu kibaya”
kumrudisha akashuka wakawa wananirudisha mimi Kinondoni, basi kufika
studio mi nikashuka lakini yule jamaa alikua kalewa akaanza kutoa shit
huna lolote, nikashuka, nikawa natembea, sa wakati natembea kuna mshkaji
akanambia mbona huyo jamaa ameshika jiwe kwa nia ya kukupiga, sa mi
nikageuka kuangalia mshkaji gani huyu anaetaka kunipiga, wale wa bajaji
kwasababu wananijua wakamuwahi , sa ile nageuka kushoto kwangu, narudi
kuangalia kulia kwangu, nakutana na pikipiki na moto ikanigonga, lakini
nilikua kwenye service road.”
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK