tangazo

Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba
---
BAADHI ya wasomi nchini wameuponda utafiti uliofanywa na Shirika
la Synovate huku miongoni mwao wakienda mbali zaidi kwa kusema:
“Ulikuwa na ajenda ya siri.”
Utafiti huo pia umepondwa na wanasiasa akiwamo Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye amesema haziamini tafiti zinazotolewa na Syonovate akidai hazina ukweli wowote.
Licha ya matokeo ya utafiti huo wa Desemba mwaka jana kuonyesha kushuka kwa asilimia 25 kwa umaarufu wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa pamoja na chama chake, lakini unaweka wazi kwamba kiongozi huyu angechaguliwa kuwa Rais kama uchaguzi huo ungefanyika sasa.
Dk Slaa anaongoza kwa asilimia 17, akifuatiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Katika maoni yao, baadhi ya wasomi kutoka taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini walieleza wasiwasi wao kuhusu usahihi wa matokeo hayo na kuhoji mbinu zilizotumika wakisema inawezekana hazikuwa sahihi.Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo ameuponda akisema haukufuata misingi ya sayansi ya siasa.
Kwa habari zaidi bofya na Endelea.....>>>>>