tangazo
Wakazi zaidi ya 50 wameandamana hadi katika Ofisi za kata ya Iganzo wakidai kupewa eneo la kufanyia biashara huku wakiwa na majembe wakimtaka mweshimiwa diwani wa kata hiyo awagawie eneo hilo kwani wamechoka kudaganywa mara kwa mara
Ni vurugu tupu
Diwani Uswege Furika (Chadema) kata ya iganzo akiwatuliza wakazi wake watulie ili awaeleze ukweli kilichotokea
Kiukweli
mambo yote anayafahamu yulee yaani akimnyooshea afisa mtendaji wa kata
hiyo kuwa anafahamu vyema juu ya kiwanja hicho cha soko
Afisa
Mtendaji wa kata Iganzo Jumapili Mwasenga amemkana mweshimiwa diwani
kuwa hana taarifa yeyote juu ya swala hilo huku akisema jamani wananchi
muulizeni vizuri diwani wenu sisi tunafanya kazi kimaandishi
Wananchi
wangu sasa sijui tufanyeje maana naona hili swala limekuwa gumu kwangu
itabidi nikae na uongozi wangu halafu nitawapa jibu
Mweshimiwa diwani tuna taka haki yetu
Mweshimiwa
diwani twende eneo la tukio ukatupatie maeneo yetu tuanza biashara
tunaomba sana baba huyo dada akimsihi mweshimiwa diwani
Mbona hamnielewi nimewaambia ngoja nikae naviongozi wenzangu tuwashughulikie swala lenu mweeeee
Wakazi
wa Iganzo baada ya kuone hawamweliwi diwani wao wakaamua kuondoka
kueleea kwenye kwenye eneo walilotakiwa kupewa ili wakajigawie wenyewe
maeneo yao
Haooo wanaondoka
Mweshimiwa diwani haamini macho yake anapoona wananchi wake wanaondoka bila ya kumsikiliza
Hili ndilo eneo walilotakiwa kugawiwa sasa wananchi hao wanachagu uongozi wao wa muda ili waanza kujigawia eneo hilo
HILI NDILO ENEO WANANCHI HAWA WATAJIGAWIA WENYEWE KWA AJILI YA SOKO BAADA YA MWESHIMIWA DIWANI KUWADANGANYA
WAKAZI
wa Mtaa wa Igodima kata ya Iganzo Jijini Mbeya wameandamana kushinikiza
kutekelezewa ahadi walioahidiwa na Diwani wa Kata hiyo ya kuwagawia
eneo kwa ajili ya kufanyia biashara.
Wakazi
hao zaidi ya 50 wameandamana hadi katika Ofisi za kata na kupokelewa na
uongozi wa kata hiyo akiwemo Diwani Uswege Furika (Chadema) na Ofisa
Mtendaji wa kata hiyo Jumapili Mwasenga huku wakiwa na majembe mikononi
wakishinikiza kuanza kugawiwa eneo hilo.
Awali
ilidaiwa kuwa Diwani huyo aliwaahidi wananchi hao kuwapa eneo kwa ajili
ya biashara ambapo aliwaambia wananchi hao kufika eneo husika asubuhi
mapema kwa ajili ya kila mtu kuoneshwa sehemu yake ambayo angefanyia
biashara zake.
Aidha
katika hali isiyokuwa ya kawaida Diwani huyo alipingana na wananchi
hali iliyozua mzozo mkali baina yake na wananchi ambapo alikataa kutoa
ahadi hiyo lakini baada ya kubanwa sana alikubali na kudai kuwa suala
hilo alilifikisha kwa Ofisa Mtendaji wa Kata.
Baada
ya Ofisa mtendaji kupewa nafasi ya kulizungusuala hilo pia alipingana
na Diwani huyo kwa madai kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa juu ya ahadi
hiyo hivyo alichokifanya Diwani huyo alipotosha wananchi.
Ofisa
huyo Jumapili Mwasenga alisema suala la Wnanchi kudai eneo la Soko ni
madai ya msingi lakini yana taratibu zake namna ya kuyapata kuongeza
kuwa kama Diwani aliahidi alitakiwa kutoa taarifa Ofisini kwake ili
walifanyie utaratibu.
Aliongeza
kuwa pamoja na ahadi hiyo bado yeye kama Mtendaji anatekeleza Ilani ya
Chama cha Mapinduzi na siyo Chama kingine hivyo Diwani alipaswa kupeleka
maombi ya wananchi kwa maandishi ili yafanyiwe kazi.
Kufuatia
majibu hayo yaliyoibua hasira kali kwa wananchi ambao walianza kupiga
kelele wakidai kuoneshwa eneo ili wakaanze kupanga meza tayari kwa
biashara ambapo Mtendaji huyo aliwaahidi wananchi kusubiri ili taratibu
zianze kufanyika ili wapewe eneo hilo.
Wananchi
hao hawakulizika na majibu ya Mtendaji huyo hali iliyopelekea kumbana
Diwani wakidai kuwa hawana imani naye kwa kuwa alikurupuka kutoa ahadi
huku akifahamu utaratibu unaotakiwa kufuatwa kabla ya kuanzishwa kwa
soko.
Godfrey
Sanga mkazi wa Mtaa wa Igodima alisema Suala la maendeleo ya kata ya
Iganzo limekuwa likipigwa danadana kila siku ambapo Diwani kupitia
mkutano wa chama cha Chadema uliofanyika Jumapili iliyopita aliwaahidi
wananchi hao kuwa wafike kwa ajili ya kupewa maeneo hali iliwalazimu
wananchi kufika eneo hilo wakiwa na majembe mikononi.
“
Wanatuona kama watoto tusiokuwa na akili huyu diwani yeye mwenyewe
aliahidi kututengenezea barabara na soko alisema lipo eneo tayari sisi
tuje ili kila mtu apewe sehemu yake lakini badala yake anatugeuka”
alihoji Hassan Kasangula mkazi wa mtaa wa Igodima.
Hata
hivyo wananchi hao walionesha kutoridhika na kauli za viongozi hao hali
iliyowalazimu kufika eneo la soko na kuchagua uongozi wa mpito na
kuanza kujigawia tayari kwa kuanza biashara huku uongozi ukibaki
unashangaa.
Aidha
kufuatia hali hiyo Diwani huyo alimtupia lawama Mwenyekiti wa Chadema
wa kata hiyo kuwa ndiye aliyetoa ahadi hiyo kwenye mkutano hali
iliyosababisha yeye kulaumiwa na wananchi akihusiashwa na ahadi hiyo.
MBEYA YETU