Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Wananchi wachukizwa na mpango wa kutorushwa live kwa matangazo ya bunge

Wananchi wachukizwa na mpango wa kutorushwa live kwa matangazo ya bunge

tangazo

bunge 012
Katika kile kinachodaiwa ni kukomesha vurugu na wabunge wanaotafuta umaarufu wa bei chee, Bunge limeanza mchakato wa kusitisha matangazo ya vikao vyake kurushwa moja kwa moja na televisheni, kama ilivyo sasa.


Badala yake linatarajia kuanzisha chaneli yake, itakayorusha yaliyojiri kwenye vikao hivyo, baada ya kuhaririwa. Uamuzi huo umepokelewa kwa hasira na wananchi wengi nchini na haya ni maoni ya baadhi yao waliyotoa kupitia ukurasa  wa Facebook.

John Kundi
Liwalo na liwe bunge la wananchi litaiwajibisha serikali endapo watafikia kutorusha vikao vya bunge,kwanI sisi ndio walipa kodi na tunastahili tuone wanajadili vipi kuhusu kero za wananchi…na wale walofanya bunge kuwa kitanda chao nao waonekane ili kuwapa wanachi urahisi wakujua mbivu na mbichi ni zipi.

Juntwa Alfred
Nadani walioleta hilo pendekezo ni wale vilaza wanaolalalala bungeni, hata sasa hawaogopi hata mwanga wa kamera,ikizimwa ndio kabsa watapeleka magodoro Dodoma.

Saba Rayup Twnbby
Kufanya hvo n upumbav wa watu walokosa fikra, unataka wananch wajueje mipango na shughul za kujenga taifa lao zaid ya kuona majadiliano ya hoja na miswada bungen? Il suala me cjalisupport ata kidogo na kufanya hvo n kupotosha jamii na kufcha maov meng zaid ya serìkal.. Ushaur wang tuendelee kuonesha bunge lakn kanun na taratbu za bunge zizngatiwe kwa wabunge ikiwezekana wanaovunja wawajìbshwe ìla co kuficha shughul za kibunge kwa wananch kwasabbu wao ndo wahucka wakuu.

Benjamin Simime

Huo ni ujinga na upotofu wa mawazo hv wabunge kuongea live ni tatizo kwakufanya hvo lengo ni kutaka kpunguza makali ya ukweli au mwishoni mtasema Parentol advised for viewers above 45 nonsense.


Jenipha Paulo
Siungi mkono point ya huyo jamaa hata kidogo wanataka ku edit eeehh wajanja hao bunge liendelee kurushwa kama kawa coz ukisema vipindi havirushi coz wanagombana itakua ni kukomoa wananchi so kama ugomvi upo utaendelea kuwepo hata wasiporusha live, hatutaki uchakachuaji warushe tuine maujinga wanayofanya hapo bungeni kama watoto.
Mwinjuma Eliah
Tukiruhusu kufanyika hivi, matangazo ya bunge kuhaririwa kwanza tutakuwa tunawanyima baadhi ya wabunge wa upinzani kuonekana na hii ni mbinu ya serikali kutokomeza upinzani tusikubali hata kidogo.Tumewachoka hatukubali hata kidogo hela zetu kuzichezea change ni mimi change ni wewe tubadilike tuungane tuwe kitu kimoja sisi sote tulio maskini …………EEEEEEEE MUNGU TUSAIDIE TUEPUSHE NA HAWA WAFILISI NA MAFISADI WA FEZA ZA MASKINI AMINA.

Dickson Onyango

Huu ni upuuzi wa hali ya juu, ivi kuna bunge linaloonyeshwa baada ya editing duniani? Uyu Makinda cjui anawaza nn na ndugu zake, wanazani unaweza kuzuia habari kwa njia za kitoto namna iyo? wabunge hawatafuti sifa yeyote bali wanasimamia haki yao inayokandamizwa na kiti (spika), tendeni haki muone kama kuna mtu atapiga kelele.


Dionest Friday uamuz mzur coz wabunge wanapenda sifa kwasabab c tunawaona wantafuta cfa za taarab bungen is gud idea. kwasabab wanaacha kilchowapeleka wanaanzisha taarab bungeni.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger