tangazo
KIJANA Peter Bosco mkazi wa Itiji, mjini Mbeya aliyedaiwa kumuua kwa kumchoma kisu kifuani mgoni wake Daniel Mwasalemba Februari 8, mwaka huu, naye amefariki dunia baada ya kupigwa kwa mawe na watu wenye hasira kali.
“Watu wenye hasira kali walimpiga kwa mawe Peter siku ya tukio na kusababisha polisi wampeleke hospitali alikolazwa baada ya kuumia, amefariki hivi karibuni na tayari ameshazikwa,” alisema ndugu huyo.
Peter anadaiwa kumuua Daniel kwa kumchoma kisu kifuani na kumburuta marehemu hadi kando ya barabara huku akiwa uchi wa mnyama baada ya kumfumania na mwanamke wake aitwaye Elizabeth Michael.
Kamanda Diwani alisema chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa kimapenzi baada ya Peter kumfuma Daniel akiwa nyumbani kwa mwanamke huyo ambapo aliwafungia mlango kwa nje na kwenda kutafuta kisu alichokitumia kumuua mwenzake.


