tangazo
Tulikua na uhakika kwamba ni
idadi ndogo ya Watanzania waliofanikiwa kununua na kuvitumia vinga’muzi
toka mfumo wa digital uanze kutumika Tanzania lakini hatukuwahi
kupata ni asilimia ngapi ya watu ambao hawatazami Tv kutokana na kukosa
vinga’muzi.
Taarifa imetufikia kwamba utafiti
wa haraka uliofanywa na umoja wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT
umeonyesha kwamba kwa Dar es salaam pekee, ni zaidi ya asilimia 75 ya
Watanzania haitazami channel za TV za nyumbani toka kuzimwa kwa mitambo
ya analog ndio maana umoja huo bado umeendelea na msimamo wa kuitaka
serikali kuangalia upya uwezekano wa kurudisha matangazo ya analog
kwanza.
Haya ni maelezo ya mwenyekiti wa MOAT
Reginald Mengi: “Watanzania wapewe muda kujiandaa ili kutoka
analog kwenda digital ifanyike vizuri na kwa mafanikio makubwa,
pendekezo letu lilikua ni kwamba analog na digital ziende sambamba mpaka
tufike mahali tuone kwamba watu wengi kama sio wote wana vyombo vya
kuwawezesha kwenda digital, hilo lifanyike kabla ya tarehe 17 june 2015
ambayo ndio siku ya mwisho ya kutumia analog”
milardayo