tangazo
Mahakama
kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 35 Samsoni
Daniel Mwang’ombe baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia
ndugu wa familia moja wapatao saba.
Akisoma
mashtaka mbele ya jaji wa mahakama hiyo Samwel Karua, Mwendesha
mashtaka wa Serikali Rhoda Ngole alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa
hilo Juni 21, 2010 kinyume cha kifungu cha 195 (16) kilichofanyiwa
marekebisho Mwaka 2002.
Ngole
aliiambia Mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo mwaka huo
majira ya 2:00 hadi saa 2:30 usiku ambapo alifika nyumbani kwa baba yake
akiwa na sigala mkononi huku akiivuta na baadaye kuidondosha sigala
hiyo iliyosababisha moto kuwasha nyumba.
Aliwataja
walioathirika na moto uliokuwa umewashwa kutokana na sigala aliyokuwa
ameidondosha mtuhumiwa kuwa ni Daniel Mwang’ombe, Anitha Richard,
Salome Mwang’ombe,Jane Samson, Diana Samson, Maria George na Cloud
Samson.
Kutokana
na kosa hilo mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na kwamba aliua bila
kukusudia ambapo alikiri kuwa akiwa anavuta sigala alidondosha kipande
hicho ambacho kilikuwa bado kinawaka moto.
Aidha
Mwendesha mashitaka huyo aliiambia mahakama hiyo kuwa pamoja na mtuhumiwa kukiri
kusababisha vifo bila kukusudia mahakama impe adhabu kali kwa mujibu wa
sheria.
Kabla
ya kutolewa kwa hukumu hiyo Wakili wa upande wa utetezi Sambwee
Shitambala alisema Mahakama inatakiwa kumwonea huruma na kumpunguzia
adhabu mshtakiwa kutokana nayeye kuwa miongoni mwa wafiwa.
Alisema
mshtakiwa ameondokewa na wazazi, watoto na mke katika ajali hiyo ambapo
hakuhudhuria mazishi yao pia amekaa muda mrefu akiwa mahabusu ambapo
amekaa kwa miaka mitatu na kuongeza kuwa mtuhumiwa ni kijana ambaye ni
nguvu kazi ya taifa hivyo hastahili kufungwa.
Na Venance Matinya, Mbeya.