Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » TID AKERWA NA UGOMVI WA CHID BENZ NA NGWAIR

TID AKERWA NA UGOMVI WA CHID BENZ NA NGWAIR

tangazo

Mashabiki wa Bongo Flava wiki hii walisikitishwa na taarifa za Chidi Benz kumpiga mshikaji wake Ngwair. Katika tukio hilo lililotokea Ambassador Lounge jijini Dar es Salaam, Ngwair alidaiwa kujeruhiwa na chupa. 

Tukio hilo lilimsikitisha pia mshkaji wao mwingine, Khalid Mohamed aka TID ambaye kwa mujibu wa U Heard ya Clouds FM, alipiga kioo cha gari yake kwa hasira.

DSC04280
“Hawa jamaa wanapigana pigana tu, me wananiudhi unajua kwanini , kwanini wao wanapigana pigana kila saa tu, huyu mara kampiga huyu and we all spend time together, at the end of the day wao wanaanza kupigana, mimi wananiconfuse, wananipotezea concentration ya kazi,” alisema TID.

“Hakuna sababu ya msingi watu wanapigana tu, watu wanongea saa zote tupo wote halafu baadae unaona watu wanaanza kupigana, unauliza sababu eti huyu kanambia mi dogo.. come on man. Mi nimewamind wote wanaopigana na ku disturb peace kwenye concentration ya kazi, violence inaonyesha sisi ni wajinga.”

Hata hivyo Chidi Benz aliendelea kusisitiza kuwa hakumpiga Ngwair. “Nani anaeamini Ngwea kapigwa? Y nimpige na ni mtu niko nae kila siiiku mabatani, tumefanya kazi nyiingi na tuna mipango,tafadhali usishabikie kitu na ukajiona mjinga mwishoni,” aliandika Chidi kwenye akaunti yake ya Facebook.

“Kuhusu swala la Ugomvi kati ya mimi na Mangwea naomba lisikuzwe ikaonekana ni sababu najua wabaya wangu watavyoweza kulikuza hili.hatuna Ubaya na ngwea na ni boonge la mshkaji..tusameheane haya Maisha tunatafuta.Peace, no lie.”
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger