tangazo
MNENGUAJI wa Bendi ya FM Academia, Suzan Chubwa ‘Queen Suzy’ amesema
hahitaji mwanaume yoyote kwa sasa kwani wanampotezea muda kwa kipindi
kirefu.
“Bora niwe singo natafuta pesa kuwazawaza hawa wanaume nitaishia kuumia tu na kushindwa kufanya shughuli zang, tena waache kunifuatafuata kwa sasa,’’ alisema Queen Suzy.
Mnenguaji huyo alishawahi kuwa na uhusiano na mwimbaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Kalala Junior ambaye alizaa naye mtoto mmoja baadaye akatembea na rapa wa FM Academia, G 7 ambao wote ameshamwagana nao.