Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » BWANA HARUSI AMUUA BABA YAKE KWA RISASI HUKO KIBAHA

BWANA HARUSI AMUUA BABA YAKE KWA RISASI HUKO KIBAHA

tangazo
Mwanaume  mmoja wa miaka 47 aliyejulikana kwa jina la Shirima mkazi wa Kibaha, amemuua baba yake mzazi anayekadiriwa kuwa na miaka 70 kwa kumpiga risasi iliyotoka kwenye bunduki yake  (short gun -"SMG")

Inasemekana baba huyo alikuwa amelala nyumbani kwa mwanae akitokea Moshi kwa mwaliko wa harusi ya bwana Shirima ambayo ilikwisha fanyikana .Siku hiyo Shirima na mkewe walikua honeymoon hapo nyumbani kwao.


Usiku wa jana baba yake alipatwa na haja ndogo akaenda chooni wakati anarudi akakosea mlango wa chumba chake na kuingia chumbani kwa mwanae....


Mke wa Shirima aliposikia mlango unafunguliwa na mtu yupo ndani,  alianza kupiga kelele za mwizi....mwiziiii!!!...,

Hapo ndo mumewe akachukua short gun yake na kumlenga babake na kumuua akidhani ni mwizi.

Inavyosemekana ni kwamba, mtaani kwao nyumba zipo mbalimbali na ndo maana akachukua uamuzi wa kumimina risasa bila kuuliza hata swali moja kwa mvamizi huyo wa chumbani kwake.


SOURCE:  WAPO RADIO ASUBUHI HII Via Jf

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger