Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » HUYU NDO MBUGE ALIYEDONDOKA JANA BUNGENI

HUYU NDO MBUGE ALIYEDONDOKA JANA BUNGENI

tangazo
MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),  Mwanamrisho Taratibu Abama  jana asubuhi aliugua  na  kuanguka ghafla katika viwanja vya Bunge na kukimbizwa hospitali....
 
Tukio hilo lilitokea wakati akienda  kuhudhuria semina ya wabunge kuhusu  Rasimu ya Sera ya Gesi Asilia kabla ya kukosa nguvu   na  kudondoka  na  kisha kusaidiwa na wenzake  kumkimbiza kwenye zahanati ya Bunge. 
 
Baada ya kupatiwa huduma ya kwanza bungeni, gari la wagonjwa lilimkimbiza Hospitali  ya Mkoa wa Dodoma (General) ambako amelazwa. 
 
Kwa mujibu wa waliomshuhudia, mbunge  huyo  alianza kwa kuishiwa nguvu hali ambayo waliokuwa karibu  walimsaidia kumpeleka kwenye zahanati ambako alitundikiwa dripu  kabla ya kupelekwa  hospitalini.
 
Kaimu Mganga Mkuu wa  Hospitali ya Dodoma,  Zainabu Chaula alikiri kumpokea mbunge huyo.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger