Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MBINU ZA KIMAHABA ALIZOZITUMIA KARRUECHE TRAN KUUTEKA TENA MOYO WA CHRIS BROWN

MBINU ZA KIMAHABA ALIZOZITUMIA KARRUECHE TRAN KUUTEKA TENA MOYO WA CHRIS BROWN

tangazo



Kwa kawaida mapenzi hutawaliwa na hisia za kimahaba alizonazo mtu kwa mwenziwe ama mtu anaetamani kuwa nae kama boyfriend/girlfriend wake ama mke/wake. Lakini hakukosea aliyesema mapenzi ni kama mmea unaweza kutunzwa na kustawi na ukiachwa bila matunzo unaweza kunyauka.



Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mrembo Karrueche Tran aliyetoswa vibaya na Chris Brown lakini kwa kuweka mikakati ya dhati na kuumwagilizia vyema mmea wa penzi kati yake na na Chris hata wakati akiwa hana muda nae na anahang out na Rihanna kumemsaidia kurudisha kwa kasi na nguvu mpya penzi alilopoteza.
 
Moja kati ya mikakati ya kimahaba aliyoitumia Karrueche huku moyoni mwake akiuamini msemo wa ‘mvumilivu hula mbivu’, ni kujiweka karibu na Chris kama rafiki hata wakati akiwa bado yuko na Rihanna na hakuonesha chuki ya wazi kwake japokuwa alikuwa anaumia sana.



Mkakati mwingine ni kuhakikisha anaonesha moyo wa upendo wa dhati na nia ya kuwa na Chris Brown kwa kuwa alijua kabisa kuwa mwisho wa siku ataangalia zaidi anakooneshwa kupendwa na kuvumiliwa, akijua mwisho wa siku akiumizwa na kulizwa huko aliko atahitaji kufutwa machozi na kutulizwa, na Karrueche atakuwa karibu zaidi, na kweli ndicho kilichotokea.



Chanzo cha karibu na KT kimesema, “Karrueche hakuwahi kuacha kumpenda Chris, hakuwa kulazimisha kitu chochote kwake kwa upande wa mahusiano, na hakuwahi kulazimisha kupewa kitu mkononi au kuomba chochote kwake.”



Mkakati huo pia ulimuongezea alama za ushindi kwa jamaa, lakini pia alijua kabisa ya Rihanna yatapita tena, kwa imani yamepita kweli. “Alijua alikuwa bado anafanya vyote na Rihanna na alitegemea hilo na muda wote alikuwa rafiki kwa Chris Breezy hata wakati akiwa na Rihanna.” Kiliendelea kufunguka chanzo hicho.



Kwa sasa KT amehamia nyumbani kwa Chris na ripoti zinasema ni takribani nusu mwezi hivi na wanaishi kama mke na mume.

LT
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger