Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » VIDEO: P- FUNK AWACHANA TENA CLOUDS FM.... AELEZA JINSI MAREHEMU NGWEA ALIVYOGUZWA NG'OMBE WA MAZIWA

VIDEO: P- FUNK AWACHANA TENA CLOUDS FM.... AELEZA JINSI MAREHEMU NGWEA ALIVYOGUZWA NG'OMBE WA MAZIWA

tangazo

Kwa mara nyingine  tena P-Funk amezungumzia sababu anazodhani zilipelekea marehemu Ngwea kujiingiza kwenye madawa. 

Producer huyo ameichana CloudsFM kwa kile anachokiona kama unyanyasaji kwa wasanii, na kwamba dhuluma za Clouds Fm ni moja wapo ya vitu vilivyosababisha maisha ya Ngwear yawe na muelekeo mbaya.

 “Ngwair alikua kama ng’ombe wenu; mnamkamua tu maziwa.”  P funk

Akizungumzia kuhusu kuikataza Clouds FM kupiga nyimbo za Bongo Records  zikiwemo wa Ngwea, P-Funk amesema:


“Niko kwenye harakati za kuandaa barua ili nistopishe nyimbo zangu zote za Bongo Records, zisipigwe Clouds Fm. 

Sababu kubwa ni uonevu wa haki miliki. Eti mnajiita  number one radio station??. Mnajidaganya .Kisaikolojia wasanii wote mmewateka. 


Wote wanaona “bila kupeleka nyimbo zao Clouds hawatafanikiwa.” Mimi cha kwanza nataka kuonyesha mfumo mwingie kwamba bila nyinyi tutaweza. Cha pili mnaingiza hela sana ya wadhamini  lakini hamui-distribute kwa wanaohusika...

"Mfumo wa kupeleka nyimbo Clouds nilianzisha mimi . Hivyo nitakua wa kwanza kujitoa na kuanzisha mfumo mwingine.” 

Video :
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger