BAADA YA VIFO VINGI, WASANII WAHAMASISHANA KUMRUDIA MUNGU
tangazo
KUTOKANA na vifo vya mara kwa mara vya wasanii, staa wa filamu za
Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ ameibuka na kusema ni wakati wa wasanii
kumrudia Mungu.
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Dude alisema kwa kipindi
kifupi vimetokea vifo vingi vya wasanii tena wenye umri mdogo, hivyo
anawataka wasanii wabadili mfumo wao wa maisha kwa kuachana na mambo
maovu, anasa za dunia kwani hawajui siku wala saa ya kufariki dunia.
“Wasanii
tunazidi kufa, juzi tumemzika Ngwea, leo tena Kashi wasanii tunatakiwa
kufanya ibada, wenye sauti za kuimba wamwimbie Mungu kwani waliotangulia
hawakujua kama watakufa, binafsi nimeanza kusali tangu nilipofiwa na
mama yangu,” alisema Dude.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK