Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , , » MIMBA YA PENNY NA DIAMOND YATOKA

MIMBA YA PENNY NA DIAMOND YATOKA

tangazo

TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja....

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
 
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.


Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.


Baada ya kupata habari hizo, mwandishig wetu alilimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:

Mwandishi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?

Mwandishi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine? 

Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.

Mwandishi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
 
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.

Mwandishi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine? 

Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.

Credit: GPL
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger