Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MTOTO AFANYIWA UPASUAJI KUONDOA MIGUU MIWILI YA ZIADA

MTOTO AFANYIWA UPASUAJI KUONDOA MIGUU MIWILI YA ZIADA

tangazo

Mtoto wa miezi miwili wa kiume nchini Namibia amefanyiwa upasuaji wa aina yake baada ya kuwa amezaliwa akiwa na miguu minne.
 

Andrew Palismwe, anayetokea Caprivi, anaendelea vizuri na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji uliochukua masaa tisa kuondoa miguu miwili kwenye Hospitali ya watoto ya Red Cross War Memorial  iliyoko mjini Cape Town, Afrika Kusini.

Mtoto huyo sasa anaendelea kupata nafuu kwenye Hospitali ya Windhoek Central nchini Namibia, imeripotiwa.

Alizaliwa akiwa na miguu miwili ya ziada chini ya tumbo lake Aprili 6. Hali hiyo inadhaniwa kuwa ni matokeo ya mapacha ambao hawakukamilika.
 

Daktari wa Hospitali ya Windhoek Central, Clarissa Pieper alisema: "Hii ni hali ambayo mapacha wameungana pamoja na kufuatia mimba ya mapacha ambayo hawakutengana kabisa, lakini kuunda watoto wawili wanaokua ndani ya kila mmoja. Katika suala hili, mtoto mwingine hauendelea kikamilifu."
 

Mama wa Andrew, Ruthy Mutanimiye alisema katika hospitali hiyo kwamba mtoto wake huyo wa kiume 'amepata nafuu haraka mara baada ya matibabu' baada ya siku nzima ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi.
 

Pia alizungumzia kuhusu faraja yake kwamba mtoto wake alifanyiwa upasuaji ambao asingeweza kumudu gharama zake.
Serikali ya Namibia ililipia gharama za upasuaji huo kupitia mfumo ambao husaidia wagonjwa wenye hali mbaya wasioweza kumudu gharama za hospitali binafsi.

Ester Paulus, msemaji wa Wizara ya Afya ya Namibia na Huduma za Jamii, alisema: "Mfuko huo ulianzishwa kusaidia wagoniwa ambao hawana njia yoyote kupata matibabu kwenye hospitali binafsi.
 

"Tunashughulikia kila ombi kwa uharaka, na kwa sasa, hakuna fomu zozote za maombi zinayosubiri kufanyiwa kazi."

Alikataa kutaja gharama za upasuaji wa Andrew, akisema: "Hakuna kiasi cha pesa kinachoweza kulinganishwa katika uokoaji maisha."
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger