Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MWIGULU NAYE ADAI KUWA BOMU LILIRUSHWA NA CHADEMA...."KAMA SIO WAO, MCHUKUA VIDEO ALITAARIFIWA NA NANI KWAMBA BOMU LITARUSHWA???"

MWIGULU NAYE ADAI KUWA BOMU LILIRUSHWA NA CHADEMA...."KAMA SIO WAO, MCHUKUA VIDEO ALITAARIFIWA NA NANI KWAMBA BOMU LITARUSHWA???"

tangazo

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba  amesema bungeni leo kwamba Chadema ilipanga kufanya shambulio la bomu kwenye mkutano wa Soweto jijini Arusha.

Amesema hakuna jambo ambalo Chadema wamewahi kupanga wakashindwa.

“Itakuaje mtu amechukua mkanda wa tukio la umwagaji wa damu bila kutikisika au mchukuaji kukimbia, haiwezekani- hiyo walipanga.

“Inakuaje amechukua mkanda wa video kama mkanda wa harusi, yaani kama mkanda wa sendoff.? Amehoji Mwigulu huku wabunge wa CCM wakimuunga mkono kwa kupiga meza bungeni.


Mapema wiki hii katika mkutano wa Chadema, mtu mmoja asiyefahamika alirusha bomu kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha watu wanne  kufariki dunia na wengine 68 kujeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mt Meru, Arusha.

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger