Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » LOWASSA APONGEZWA NA BAKWATA KWA KUVISHWA JOHO MAALUMU.....MILIONI 590 ZACHANGISHWA KATIKA HARAMBEE

LOWASSA APONGEZWA NA BAKWATA KWA KUVISHWA JOHO MAALUMU.....MILIONI 590 ZACHANGISHWA KATIKA HARAMBEE

tangazo

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akipongezwa na kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al Badawi kwa kumvika joho la kilemba  baada ya kufanikisha harambee kwa ajili ya Kituo cha Redio Ikra kinachomilikiwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza. 


Anayeshuhudia ni Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Sheikh Salum Hassan Fereji. 


Katika harambee hiyo zaidi ya sh. mil. 590 zilipatikana na kuvuka lengo ambalo lilikuwa sh. mil 500. 




WAZIRI Mkuu mstaafu  Mhe.Edward Lowassa ijumaa usiku aliongoza harambee kubwa  na ya kihistoria ya kuchangia kituo cha Redio IQRA Fm kinachomilikiwa na Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza (BAKWATA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest Jijini Mwanza.



Mhe.Lowassa aliyekuwa Jijini Mwanza kushirikiana na marafiki zake, wafanyabiashara, taasisi na  makampuni mbalimbali, watu binafisi na viongozi wa serikali na vyama vya siasa na wabunge wa majimbo mawili ya jijini Mwanza Ilemela na Nyamagana kupitia CHADEMA yaliyotuma wawakilishi wao hatimaye aliweza kuvuka lengo lililowekwa kwa kukusanya zaidi ya shilingi milioni 590 zikiwemo ahadi.
















TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger