Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » "MAMA YANGU HAKUSTAHILI KUFARIKI .....ALIKUWA BADO NI KIJANA SANA "..BARNABA

"MAMA YANGU HAKUSTAHILI KUFARIKI .....ALIKUWA BADO NI KIJANA SANA "..BARNABA

tangazo

Muimbaji wa THT Barnaba Elias amesema mama yake mzazi amefariki mapema mno na akiwa na umri mdogo. 
 
Msanii huyo ambaye yeye na Amini wanaunda kundi liitwalo Gemini alikuwa akiongea na Bongo5  leo na  kudai  kwamba  wimbo wao mpya ‘Why Mimi’ una uhusiano na msiba huo wa mama yake aliyefariki mwezi uliopita.

“Mimi mama yangu obvious nilikuwa nampenda sana. Mama yangu ndio mtu ambaye alisababisha Barnaba na ndio nimesimama hapa mnaniona Barnaba,”alisema na kuongeza



“Mzee yupo lakini power nyingi niliipata kwa mama, wote walikuwa wananisaidia vizuri lakini mama nilimzoea kwasababu mama alikuwa kipenzi changu zaidi ya kipenzi, mshkaji wangu zaidi ya mshkaji rafiki yangu wa dhati.


"Nilikuwa na uwezo wa kumwambia vitu vyangu vya ndani, nikamshirikisha akanisaidia, akanipa mawazo, tukataniana, tukacheka. Kwahiyo ni vigumu, ni neno ambalo huwa linarudi lakini siwezi kumkufuru mwenyezi Mungu.
 
"Ni neno ambalo huwa najiuliza why mimi? Sababu mama yangu amefariki akiwa kijana sana na ni ghafla sababu mama yangu mimi hakuumwa, kafa tu pressure, kwikwi, akapoteza maisha.”

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger