Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » UGOMVI WA NDOA WASABABISHA MWANAMKE AVAMIWE NA KUKATWA MIKONO YAKE

UGOMVI WA NDOA WASABABISHA MWANAMKE AVAMIWE NA KUKATWA MIKONO YAKE

tangazo

Mwanamke mmoja Sumayi Girandi mkazi wa kijiji cha Kunzugu wilayani Bunda amepoteza vidole vitatu vya mkono wa kulia na kiganja cha mkono wa kushoto kukatwa baada kushambuliwa kwa mapanga na watu wasiojulikana kisa kikidaiwa kuwa kutaka kunyang’anywa mali zake.


Uhodari wa mama huyo wa kutafuta mafanikio ya familia yake hasa baada ya kutengana na mume wake umeishia hapo baada ya watu wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake na kumshambulia kwa mapanga na kisha  wakamkata kiganja cha mkono wa kushoto na kuanguka.


Kwa sasa Sumayi Girandi anatibiwa katika Hospitali teule ya wilaya.

Vitendo vya kujeruhi na kuua wanawake mkoani Mara kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo ya ndugu kutaka kuwanyang’anya bado vinaendelea.

Katika tukio lingine wilayani Bunda dereva mmoja wa pikipiki ameuawa na watu wasiojulikana ambapo taarifa zinasema kuwa kabla ya kuuawa kwa dereva huyo wa bodaboda inadaiwa alikodiwa na watu wawili.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mara Ferdinand Mtui amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na tayari watu wanne wamekamatwa wakiwemo watu wanaotuhumiwa kumkatakata mapanga mwanamke Sumayi Girandi.

Emmanuel Amas, TBC Mara.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger