Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Basi la Turu lachomwa moto na wanakijiji....Abiria 60 wamenusurika

Basi la Turu lachomwa moto na wanakijiji....Abiria 60 wamenusurika

tangazo
 
Abiria wapatao 60 waliokuwa wanasafiri na basi la Turu linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Singida na Haidom mkoani Manyara, wamelazimishwa kuteremka toka ndani ya basi hilo na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 ) wa vijiji vitatu, na kisha kulichoma moto basi hilo.

Taarifa toka eneo la tukio zinasema wananchi hao ni wa vijiji vya Singa, Idabagadu na Nkungi mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria wote wameshuka, walilichoma moto basi hilo ambalo limetekea sehemu kubwa.

Sababu ya wananchi hao kuchukua uamuzi huo ni kutokana na basi hilo kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger