Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » UJUMBE WA RAY C KWA WAVUTA BANGI WOTE...

UJUMBE WA RAY C KWA WAVUTA BANGI WOTE...

tangazo


Ray  C   ambaye aliathirika na matumizi ya dawa za kulevya na baadae kupona  ameendelea kuwa kioo cha jamii kwa ku-share experience yake baada ya kupona kwenye ishu ya dawa za kulevya. 


Msanii  huyo  ametoa ujumbe mpya ambao ni muhimu kila mtu kuujua kwasababu kwenye mazingira yetu kuna waathirika wengi wa dawa za kulevya.
 
Haya ndiyo maneno ya Ray C mwenyewe ambayo yana ujumbe mzuri ndani yake:

“Wote hawa tuliokaa hapa(picha hapo chini) tuliathirika na dawa za kulevya na tumepona kwa kunywa dawa moja tu inayoitwa Methadone. Inapatikana Muhimbili na Mwananyamala pekee na ni bure kabisa.
 
"Tunamshukuru sana Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutuletea dawa hii.Ningependa kuwashauri walioathirika wa dawa za kulevya iwe wewe,ndugu  yako,rafiki,kaka,dada,mjomba,jirani au yoyote aliye karibu na wewe.

"Usiogope amua tu kwamba unataka kupona na nenda kanywe hii dawa utapona kabisa.”

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger