tangazo

Watu sita wamefariki dunia na wengine 34 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Chinangali wilayani Chamwino mkoani Dodoma baada ya basi la kampuni ya Al Sayeed lililokuwa likitokea jijini Dar-Es-Salaam kwenda Dodoma kugongana uso kwa uso na lori la mizigo lililobeba shehena ya mahindi likitokea Dodoma kwenda Dar es salaam.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kaimu kamanda
wa polisi mkoa wa Dodoma Mrakibu Mwandamizi Damas Nyanda amesema chanzo
cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo lenye namba za
usajili T 433 BLR aina ya Youtong ambaye alishindwa kulimudu na kuacha
njia na kulivaa lori aina ya Layland Daf lenye namba za usajili T 102
CGR likiwa na tela lenye namba za T 928 na kusababisha watu watano
kufariki papo hapo.
ITV ilifika katika eneo la tukio na kuzungumza na
baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo na wamelalamikia uhaba wa vyombo vya
uokoaji ambapo wamesema kama vyombo vya uokoaji vingefika kwa wakati
huenda watu wote wanne waliofariki kwenye lori wangeokolewa.