Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » JESHI la Kenya limeamua kulipua sehemu ya jengo lililotekwa ili kuwakabili WAASI wa AL SHABAAB

JESHI la Kenya limeamua kulipua sehemu ya jengo lililotekwa ili kuwakabili WAASI wa AL SHABAAB

tangazo

BBC  wamearifu  kuwa vikosi vya usalama vimezingira jengo  lililotekwa  na  waasi  nchini  Kenya  na hata kudhibiti sehemu ya jengo zima. 

ZIFUATAZO  NI  LIVE  UPDATES:


14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti hali na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka



14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo
13:54: Mwandishi wa BBC Idriss Situma aliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo


13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao


13:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha


13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao idadi yao haijulikani

13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab

12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za mwisho
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger