Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MAITI YAFUKULIWA NA KUTUPWA NJE YA MGAHAWA JIJINI MWANZA.

MAITI YAFUKULIWA NA KUTUPWA NJE YA MGAHAWA JIJINI MWANZA.

tangazo
Jeneza la mwili wa mtoto ambalo lilikutwa limetelekezwa mbele ya mlango wa mgahawa wa Ester.
---
JENEZA lenye mwili wa mtoto mchanga, limezua taharuki kwa wananchi na wakazi wa Mtaa wa Ihago, Kata ya Mahina, Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.


Tukio hilo la kushangaza na la aina yake, lilitokea Agosti 29, mwaka huu, majira ya saa 12:00 asubuhi baada ya kugunduliwa na mfanyabiashara Ester Musa (28) likiwa limetelekezwa kwenye mlango wa mgahawa wake.
 Jeneza likiwa limefungwa tayari kwa kwenda kuzika mara ya pili.
--

Jeneza hilo linaaminika kufukuliwa na watu wasiofahamika kwenye moja ya makaburi eneo la Mahina jijini hapa.



Akizungumza kuhusiana na tukio hilo, Ester anayemiliki na kuendesha mgahawa alisema, alifika katika eneo lake hilo la biashara, ghafla akapigwa na mshangao baada ya kuona jeneza likiwa mbele ya mlango wa mgahawa wake.
Umati wa watu uliofika kushuhudia tukio hilo.

“Nashindwa kujua nini maana ya tukio hili sababu hivi karibuni nilikuta barua imebandikwa ukutani ikinitaka nihame kutoka eneo hili, vinginevyo nitaona nitakachofanyiwa. Leo nimekuta jeneza mlangoni,” alisema Ester na kuongeza;



“Tukio hili nalihusisha na imani za kishirikina lakini kubwa linachangiwa na wivu wa kibiashara.Tangu lizaliwe sijawahi kuona jambo kama hili. Hapa sijawahi kugombana na mtu yeyote nashangaa kufanyiwa kitendo cha namna hii katika eneo la biashara yangu.”
Difenda ya polisi ikiondoka eneo la tukio na jeneza hilo kuelekea makaburini.
--

Mwenyekiti wa mtaa huo, Anthony Deus alisema kitendo cha kufukua mwili wa marehemu tena mtoto mchanga, si cha kibinadamu na ni tukio la kusikitisha katika jamii, hivyo watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.



Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, ACP Christopher Fuime, alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kusema hakuna mtu aliyekamatwa akihusishwa nalo.
 Mwili wa mtoto ukizikwa mara ya pili.
--


“Tunaendelea na uchunguzi lakini hadi sasa hakuna aliyekamatwa akihusishwa na tukio hili la kusikitisha… wananchi wameuzika upya mwili wa mtoto huyo,” alisema
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger