RWANDA YANYWEA...MALORI YA TANZANIA YARUHUSIWA KUPITA KWA TOZO YA ZAMANI.
tangazo
Naibu
Waziri wa Uchukuzi Dk. Tzeba amethibitisha kuwa Serikali ya Rwanda
imeruhusu malori ya Tanzania yaendelee na safari kwa kulipa dola 152
badala ya 500 zilizoanza kutozwa hapo jana.
Akiongea toka mkoani Dodoma, Tzeba ameweka wazi kuwa Waziri wa Fedha wa Rwanda aitwaye Gatete na wa waziri wa Uchukuzi wa Rwanda aitwaye Rwakabamba, wameridhia tozo ya dola 152
iendelee kutumika.
Tzeba amedai kuwa ofisa mmoja katika Wizara ya Fedha ya Rwanda ndiye aliyekurupuka na
kutangaza mabadiliko hayo kwa mdomo.
Waziri wa Fedha wa Rwanda alipoulizwa
na mwenzake wa Tanzania, alishituka na kuahidi kulipatia ufumbuzi tatizo hilo ambapo ndani ya muda mfupi jibu lilipatikana kuwa agizo la
ofisa huyo wa Rwanda halikuwa halali.
Mbali na kauli ya Tzeba, habari za CHUMBANI ambazo mpekuzi wetu amezipata zinadai kwamba uamuzi huu umefikiwa na serikali ya Kagame baada ya Mamlaka Ya Mapato Tanzania (TRA)
kulazimika kupunguza ushuru wa barabara ( Road Toll) kwa magari yenye
plate numbers za Rwanda kwa asilimia 170.
Kwa hali hii, ni dhahiri kuwa huu utakuwa ni ushindi mkubwa kwa Rwanda ikizingatiwa kuwa
umbali kutoka Dar es Salaam mpaka Rusumo ( mpakani )sio sawa na umbali kutoka Rusumo mpaka
Kigali.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK