Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Serikali yabariki TANESCO kupandisha bei za umeme....Naibu waziri adai kuwa atakayeshindwa kumudu gharama hizo basi atumie kibatari

Serikali yabariki TANESCO kupandisha bei za umeme....Naibu waziri adai kuwa atakayeshindwa kumudu gharama hizo basi atumie kibatari

tangazo
 Naibu Waziri wa umeme, Mh George Simbachawene, amesema kwamba serikali imekubali TANESCO waongeze gharama za umeme kwa 68% kama walivyokuwa wameomba.
 
Simbachawene ameitoa  kauli hiyo wakati akiongea katika kipindi cha Kumepambazuka kupitia Radio One leo asubuhi. 


Amesema kwamba hata kama TANESCO wakiongeza gharama za umeme hadi kufikia Tsh 800 kwa unit bei hiyo ni nafuu kuliko gharama za kununua mafuta ya taa.
 
Mh Simbachawene ametahadharisha kwamba kama mtu ataona kwamba gharama za umeme ni kubwa, basi akawashe kibatari au akae gizani.
 
Source: Jamiiforum  via Kumepambazuka, Radio One.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger