Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Snura Mushi na Mrisho Ngassa wanaswa wakitomasana hadharani....

Snura Mushi na Mrisho Ngassa wanaswa wakitomasana hadharani....

tangazo

Staa wa sinema na muziki Bongo, Snura Anton Mushi na Kiungo Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa wamenaswa ‘laivu’ wakiwa kimahaba......

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lililijiri hivi karibuni nyumbani kwa Snura maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambapo wawili hao walibambwa wakiwa wamejiachia ‘wakifanya yao’.

Mnyetishaji huyo alidai kuwa wawili hao walikuwa wakiminyana bila kujali macho ya watu waliokuwa wakifika nyumbani kwa Snura hasa marafiki na majirani zake.
“Yaani walikuwa wakioneshana mahaba kama njiwa bila kificho chochote. Kuna ‘taimu’ Snura alikuwa akimpakata Ngassa utadhani mtoto mdogo.
 
“Baadaye hata Ngassa naye alifanya hivyohivyo huku akicheza na nywele za Snura anavyotaka,” alidai shuhuda wetu.
 
Ili kujiridhisha, Tulisaka picha za wawili hao ambazo walikuwa ‘wakijifotoa’ kwa simu zikiwaonesha wakiwa katika mahaba jambo lililozua utata na maswali kwa walioziona.
Uchunguzi ulibainisha kuwa siyo mara ya kwanza kwa Snura na Ngassa kunaswa wakiwa beneti kwani wiki mbili zilizopita walibambwa kwenye ukumbi mmoja wa starehe jijini Dar wakila bata ndefu.
 
Baada ya kulishwa  habari hizo,Tulimsaka Snura ambapo alipopatikana alitakiwa alimwagiwa habari yote juu ya uhusiano wake tata na Ngassa ambapo alikuwa na haya ya kusema:
 
“Nimeshtuka sana kusikia hizo picha zimewafikia kwa sababu mimi na Ngassa ni marafiki na yeye (Ngassa) ni shabiki mkubwa wa nyimbo zangu.


“Ngassa alinitembelea kama marafiki wengine wanaokuja nyumbani kwangu. Simu yangu ilipotea ndiyo maana picha zikavuja lakini ukweli ndiyo huo.”
 
Kwa upande wake Ngassa ambaye yupo mapumzikoni baada ya kumalizika kwa msimu wa kwanza wa Ligi Kuu Bara hakuweza kusema chochote kufuatia simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.

Credit: Vituko vya mtaa
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger