Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » Katibu wa chama cha madaktari ajiuzulu wadhifa wake na kujiunga CHADEMA

Katibu wa chama cha madaktari ajiuzulu wadhifa wake na kujiunga CHADEMA

tangazo

MAKAMU wa Rais wa Chama cha Madakatri Tanzania (MAT), Dk Rodrick Kabangila, amejiuzulu nafasi hiyo na kuelekeza nguvu kwenye uteuzi mpya wa kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Ziwa Magharibi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema).
 
Akizungumza jana Dar es Salaam, Kabangila alisema amefanya uamuzi huo bila kushurutishwa na anaamini kwa kufanya hivyo ataondoa mgongano wa kimaslahi kati ya vyama anavyoongoza, madaktari na Chadema.
 
Alisema pia uamuzi huo utamsaidia kuchangia kwa karibu mawazo ya kitaaluma ndani ya Chadema ambayo ana uhakika itayafanyia kazi kwa manufaa zaidi katika kuboreshaji wake wa sekta kutokana na chama hicho kuwa katika wakati wa kuandaa sera mbalimbali zikiwamo za afya.
 
Kabangila alisema uamuzi huo ameufikia baada ya kuona mawazo ya kuboresha sekta ya afya yanayotoka kwenye vyama vya kitaaluma, hayafanyiwi kazi.
 
“Kuna mambo mengi hayaendi vizuri ambayo ni ya kimfumo katika Serikali ambayo yanaendelea kudidimiza huduma za afya. Mfano urasimu katika usambazaji wa dawa na vifaa tiba, utoaji wataalamu, uzembe kuanzia wizarani na hata kutopelekwa kwa ruzuku mahospitalini,” alisema

Mbali na nafasi ya Makamu wa Rais wa MAT, Kabangila pia alikuwa Makamu wa Rais wa Shirikisho la Vyama vya Kitaaluma vya Afya na Katibu Mkuu wa kwanza wa Chama cha Wafanyakazi Madaktari na Wafamasia Tanzania (TMDPWU).
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger