Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » VIDEO: NDOA YA KWANZA YA KIMILA YA MASHOGA YAFUNGWA HUKO AFRIKA KUSINI KWA SHANGWE NA MABUSU KIBAO

VIDEO: NDOA YA KWANZA YA KIMILA YA MASHOGA YAFUNGWA HUKO AFRIKA KUSINI KWA SHANGWE NA MABUSU KIBAO

tangazo

KATIKA hali isiyo ya kawaida kwa mila zetu waafrica,vijana wawili Tshepo Cameron Modisane na Thoba Calvin Sithole  wamefunga Ndoa ya jinsia moja almaarufu kama "GAY MARRIAGE" huko mjini KwaDukuza  ulioko KwaZulu-Natal, South Africa na kuwa tukio la kwanza barani Africa kuwahi kutokea.

Habari zaidi zinadai wanandoa hao awali walikuwa na mahusiano ambayo kila mmoja katika mji huo alikuwa akiyatambua....Umaarufu wa uhusiano wao ulisababishwa kituo cha Televion cha KZN ambacho kimekuwa kwa muda mrefu kikiyatangaza mahusiano yao....



"Kwa muda mrefu tumejaribu kuuonyesha uhusiano wetu huu mbele za watu ili wale ambao walikuwa wanajificha na kuogopa waweze kuiga mfano mzuri ambao tumeuonyesha kwani ni kitu kizuri kama umempenda mpenzi wako na kuamua kudhihirisha hilo katika halaiki ya watu  " alisema Tshepo ambaye alionekna kuwa na furaha kupita kiasi na  kuongeza:

Sithole

"Tumeona hakuna haja wa kutokuwepo kwa Ndoa za namna hii huku kwetu(AFRICA), na Ndoa yetu ni Alama kwa ulimwengu kwamba Mashoga wanaweza kuoana na kutengeza familia yenye maadili yote tofauti na watu wanavyofikiria"

Wedding
Kwa upande wa Thoba , yeye  alikuwa  na  machache: "Hivi ndivyo jinsi ambavyo tumeamua kuwa, na Tumechochwa na maneno mengi ya watu ambao wamekuwa  wakipinga Ndoa hii katika bara letu hili la Africa"

Wanandoa hao walimalizia Tukio la kihistoria katika maisha yao kwa mabusu moto moto huku wakishangiliwa na watu lukuki.

ANGALIA VIDEO YA NDOA HIYO HAPO CHINI:

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger