Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » HALI YA MSANII MATUMAINI ANAYEPENDA KUIGIZA NA KIWEWE NI MBAYA

HALI YA MSANII MATUMAINI ANAYEPENDA KUIGIZA NA KIWEWE NI MBAYA

tangazo


HALI ya msanii wa maigizo Tanzania anayejulikana kwa jina la Matumaini  si ya kuridhisha kutokana na kusumbuliwa kwa maradhi akiwa nchini Msumbiji

Kutokana na hali yake ya kiafya kuwa mbaya baadhi ya watanzania waishio Msumbiji wamejitolea kumchangia nauli ili aweze kurejea nyumbani kwa ajili ya kupata matibabu na uangalizi zaidi wa ndugu zake

Akizungumza jijini Dar es Salaam mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waigizaji Mkoa wa Kinondoni , Kaftany Masoud alisema kuwa amepokea taarifa juu ya ugonjwa wa msanii huyo ingawa haijawekwa wazi anasumbuliwa na tatizo gani mpaka sasa

Alisema kutokana na hali kuwa mbaya baadhi ya watanzania wameamua kumchangia msanii huyo ili aweze kurejea nyumbani ili taratibu za matibabu zifwatwe

"Ni kweli hali ya msanii mwenzetu si nzuri anaumwa na unajua ugonjwa wa mtu unathibitishwa na Dokta hivyo bado hatujajua anaumwa nini ila tumeipokea taarifa hiyo na juhudi zinazofanywa ili kumrudisha nyumbani " alisema Masoud

Aliongezea kuwa kwa upande wao kwa sasa wapo katika mchakato wa kuchangishana fedha kwa ajili ya matibabu ya msanii huyo atakapofika hapa nchini

Matumaini ni msanii kwenye upande wa uchekeshaji. alianza kazi hiyo katika kundi la Kaole na kujipatia umaarufu kwa kuigiza na msanii mwenzie Kiwewe
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger