Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , , » JACKLINE WOLPER NA IRENE UWOYA NDANI YA BIFU ZITO

JACKLINE WOLPER NA IRENE UWOYA NDANI YA BIFU ZITO

tangazo

BODIGADI wa mwigizaji kiwango Bongo, Irene Uwoya, aliyetajwa kwa jina moja la Mariam anadaiwa kumshushia kipigo mwigizaji Jacqueline Wolper chanzo kikidaiwa kuwa ni mwendelezo wa bifu lililokuwa limefifia kati ya mafahari hao wa sinema za Kibongo.

Kwa mujibu wa chanzo makini, sheshe hilo lilitokea Desemba 31, mwaka huu  katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar, wakati mastaa mbalimbali walipokuwa wakisherehekea kuupokea Mwaka Mpya wa 2013.


Chanzo hicho makini kiliweka wazi kuwa, wakati shamrashamra za mwaka mpya zikiendelea, ghafla bodigadi huyo wa Uwoya, alimvaa Wolper aliyekuwa anacheza muziki na kuanza kumvuta cheni yake kisha kumshushia kipigo kizito.

“Mariam na Uwoya walikuwa wamekaa pamoja wakipiga kilevi na kustorisha, ghafla tukashangaa mpambe huyo ameinuka na kwenda kumvaa Wolper ambaye alikuwa bize kucheza muziki,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Uwoya atakuwa kamtuma kwa sababu haiwezekani wakae wote halafu dakika chache mbele, ainuke na kwenda kumfanyia fujo mwenzake (Wolper). Hapa kuna kitu.”

Tofauti na ilivyodhaniwa na wengi kwamba bodigadi huyo alitumwa na Uwoya, baada tukio hilo Klabu ya Bongo Movie Unit iliitisha kikao cha dharura ambapo ilidaiwa kuwa Uwoya alikana kuhusika na akamlaani Mariam kwa kitendo hicho cha kumfanyia vurugu Wolper.

 “Wasani wengi walijua Uwoya ndiye aliyetengeneza mchongo mzima lakini kikao kimekataa na kumuona Mariam ndiye mkosaji,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kusikia maelezo ya kikao cha klabu, mwandishi wetu alimtafuta Wolper na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alijibu kwa kifupi:

“Siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo, watafuteni viongozi wetu,” alisema Wolper.


Kumbukumbu inaonesha mwaka jana, mastaa hao waliwahi kuwa ndani ya bifu zito ambapo baadaye walipatanishwa na mdau wa burudani maarufu kwa jina la Daudi Kipunguni maeneo ya Mlimani City jijini Dar.
CREDIT:  GPL
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger