Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Showing posts with label Jackline Wolper. Show all posts
Showing posts with label Jackline Wolper. Show all posts

JACK WOLPER AMJIBU MBAYA WAKE ALIYETANGAZA KUWA YEYE NI KAHABA

 
Msanii  nyota  wa  filamu  bongo, Jacqueline Wolper   amewataka  wasanii wa  bongo  movie  kuacha  tabia  ya  kupigana  majungu  ya  kinafiki  ambayo  huchangia  kujenga  bifu  za  kijinga....

Akiongea  na  mpekuzi  wetu, wolper  alidai  kuwa  kuna  mipaka  ya  watu  kuishi  lakini  kuna  baadhi  ya  wasanii  wanaamini  kwamba majungu  ndo  mshahara  wao  kiasi  kwamba  wasipomsengenya  mtu  basi  hawawezi  kuishi...

Wolper  anadai  kuwa   yeye  ni  miongoni  mwa  wasanii  wanaosemwa  sana  kwa  mabaya  hasa  kuhusu  maisha  yake  ya  kila  siku.Hali  hiyo  inatokana  na  umaarufu  alionao  ambao  huwafanya   wasanii  wenzake  wamchukie  hasa  wasanii  wa  kike...



  Hii  ni  kauli  ya  Wolper  alipoongea  na  mpekuzi:

"Wasanii  tungekuwa  na  ushirikiano  kama  nisha  tungefika  mbali  sana.

"Mimi  simuogopi  mtu  katika  maisha  yangu, lakini  ninachohitaji  katika  maisha  yangu  ni  Heshima.

"Ukiona  nimekukwaza, basi  njoo  nyumbani  au  nambie  nikufuate  ili  tuyamalize  kibinadamu  na  si  kudhalilishana  mitandaoni...

"Kuna  msanii  mmoja  wa  kike  amekuwa  akinichafua  sana  mitandaoni   kwa  kuniita  kahaba, najuza  na  matusi  mengine  kibao.

"Huyo  ni  mtu  anayetafuta  pakutokea, anatafuta  kujulikana  kupitia  Wolper  na  pengine  kafulia  na  sasa  anatafuta  mtaji.

"Tangu  anitukane  sikuona  haja  ya  kumjibu  kutokana  na  heshima    niliyo  nayo  katika  kazi  yangu  na  heshima  yangu  kwa  wazazi , ndugu  na  jamaa.

"Niliamua  kumwachia  mungu.Kama  ni  kahaba  au  najiuza, mungu  anajua.Alisema  Wolper 
TUPE MAONI YAKO

"NIPO TAYARI KUPIGANA NA JACK WOLPER ENDAPO ATAENDELEA KULITUMIA JINA LANGU KUJIPATIA UMAARUFU"...BABY MADAHA


Staa  wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph ‘Baby Madaha’ ameomba pambano la ngumi dhidi ya Jacqueline Wolper ili waweze kumaliza ubishi wa bifu lao.


Akipiongea na  mwandishi wetu, Baby alisema amechoshwa kusikia tambo za mpinzani wake huyo hivyo kama kweli ni mwanamke, wakutane kwa  ngumi  ili amuoneshe cha mtema kuni.

 “Asiniambie mimi natafuta kiki, mimi ni msomi kuliko yeye, arudi shule au akauze vipodozi. Najua kuimba, kuigiza na ni msomi yeye anaweza hayo? 


"Kimsingi naomba pambano nimtoe  manundu.Nipo  tayari  kupigana  naye  ili  nimshikishe  adabu,” alisema Baby Madaha.
TUPE MAONI YAKO

JACK WOLPER ADAI KUWA ANAPENDA KUTEMBEA NA "SERENGETI BOYS" KWA SABABU WANAYAJUA MAPENZI UKILINGANISHA NA WATU WAZIMA WENYE PESA ZAO


Nyota wa tasnia ya filamu , Jaqueline Wolper ‘Wolper Gambe’ amedai kuwa hawapendi sana wanaume wenye fedha kwani wengi wao ni waume za watu...

Wolper anadai kuwa nao si rahisi kuonyeshwa mapenzi yao ya dhati  kwani mapenzi yao ni ya  chumbani tu...


" Unajua unapokuwa na mtu mwenye fedha zake , alafu mtu mzima, ni  lazmia  ukose  penzi la kweli kwani mapenzi yenu ni chumbani tu, hamuwezi kutembea pamoja kukaa kama vile ni wapenzi ...


"Lakini ukiwa na kijana ambaye hana pesa na wewe una kazi lazima akuonyeshe jinsi mapenzi yalivyo kwa kukuweka karibu kimahaba na wewe ukafaidi penzi kutoka kwake..

“Wanaume wengi wenye  pesa zao huniona  nina dharau, lakini mimi ni binadamu nahitaji haki yangu kama mwanamke .
 
"Kuna watu wanaamini pesa zao ndio kila kitu, kiukweli kwangu siyo hivyo , ukileta mapenzi hayo lazima unione nina dharau”,anasema Wolper Gambe.

Wolper  anadai kuwa  kuna watu ambao huwanyooshea vidole wasanii maarufu kama yeye kwa kuwaona kama vile ni Malaya lakini wanasahau kama nao ni binadamu na wanaroho kama wanadamu wengine....
 
Jack Wolper anasema wao si malaika , wanapenda na kupendwa, kwa hiyo ukimuona ana kijana Serengeti boy ujue ni kwa ajili ya kupata penzi nzito na kusikilizwa haja zake.
TUPE MAONI YAKO

JACKLINE WOLPER NA BABY MADAHA WASHIKANA MASHATI WAKIGOMBANIANA NYUMBA YA KUPANGA



Sakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo kumfanya awe na haki ya kuhamia.
 

Akizungumza na mwandishi wetu, juzi jijini Dar es Salaam, Madaha alisema pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni tatu) ni Wolper lakini anamchenga.

“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii mwenzangu alikuwa na uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini nimemwambia, ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa. Milioni tatu ndugu yangu si pesa ndogo.”


KAULI  YA  WOLPER

Wolper alipotafutwa na kusomewa malalamiko ya Madaha alisema: “Naweza kusema Madaha hana akili, ni mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara nyumbani kwangu tungezungumza na baba mwenye nyumba tukajua namna ya kumsaidia.

“Lakini yeye kabla hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa eti nimemtapeli. 

Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
 

“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper.
TUPE MAONI YAKO

JACK WOLPER AKANUSHA KUTUPIWA VITU VYAKE NJE BAADA YA KUSHINDWA KULIPIA KODI YA NYUMBA

 


Baada ya story ya mwanadada Jacqueline wolper kutolewa nje pamoja na vitu vyake kuzagaa kwenye vyombo vya habari hususani magazeti, tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili tupate ukweli wa jambo hilo na kuamua kumtafuta hewani


Mwandishi: Mambo Jack, mzima wewe? Jacqueline Wolper: Mi mzima, vipi salama?


Mwandishi: Salama kabisa, vipi kuhusu hii habari ya kutolewa vitu nje ya nyumba? Nini tena kimetokea?


Jacqueline Wolper: Hiyo habari sio ya ukweli kama ilivyo, ukweli ni kwamba  sijatolewa vitu ila nimehama sehemu niliyokuwa nakaa na kuhamia sehemu nyingine


Mwandishi: Kitu gani kilitokea mpaka kukawa na hizi habari za kutolewa vitu nje? Na ulikuwa unakaa wapi?


Jacqueline Wolper: Mwanzo nilikuwa nakaa ,Mbezi beach, kwenye apartment ya kama USD 1500 kwa mwezi, na nilikuwa nakaa mwenyewe, na kama unavyojua huwa nawalea wadogo zangu na muda huo walikuwa wapo chuo. Ila walipomaliza nikaona badala ya mimi kukaa mwenyewe ni bora nitafute nyumba nyingine mbili ili wakae wenyewe na mimi nikae mwenyewe. 

Ndo maana nikahama huko mbezi beach. Sa sijui hao wanaosema nimetolewa vitu nje wanatoa wapi hayo maneno. Labda kama walipiga picha wakati nahama na kuamua kujitengenezea stori.


Mwandishi: Unahisi ni kwanini wameandika kuwa umetolewa vitu nje?

Jacqueline Wolper: Mmmh! Siwezi kujua na wala hainisadii, maana sio kweli. Mi sukuona sababu ya kulipa hizo hela kwa mwezi wakati naweza kukaa kwenye nyumba nzuri ya $800 au mia $900 kwa mwezi na nikawatafutia wadogo wangu nyumba nao wakae kwa gharama hiyo hiyo na kwa uhuru wao. 
 

 Kwangu mimi haina maana hata kidogo kwa sasa kulipa hela zote bila sababu, Wakati nipo mwenyewe ilikuwa sawa ila sasa it doesn’t make sense at all. Kuna mambo mengine ya muhimu ya kufanya. Na isitoshe suala la foleni. So sijui waliondika hivyo wanatafuta nini kwangu.
 

Mwandishi: Basi tunashukuru sana Jack kwa maelezo yako.
 

Jacqueline Wolper: Asanteni sana




JUU ni baadhi ya Picha za nyumba anayoishi jackline wolper sasa baada ya kuhama mbezi
Bongomovie

TUPE MAONI YAKO

"UREMBO SIYO KIPAJI NA SI KILA MWANAMKE MZURI ANAWEZA KUIGIZA"...JACKLINE WOLPER


Muigizaji Jacqueline “Jackie” Wolper amewashangaa wanaodhani kuwa urembo wa mwanamke ni mbadala wa kipaji hasa katika sanaa ya maigizo. 




Alisema urembo ni moja ya sifa ya mwanamke lakini kamwe hauwezi kumfanya asiye na kipaji kuwa nacho.
 

“Ukiwa mrembo ni bora zaidi,kwa kuwa itamfanya avutie kwenye movie,lakini pamoja na hayo ni lazima awe na uwezo wa kuigiza kulingana na kipande husika”alisema Wolper.
 

Wolper aliendelea kulalama kuwa kila mtu akijona ana sura ya kuvutia na umbo zuri basi anajua anaweza kuigiza ndio maana matokeo yake wanafanya vitu sivyo na mwisho wake wanaacha fani kabisa.
 

Alifafanuwa kuwa kuigiza ni zaidi ya urembo hivyo yeyote ambaye anafikiri anaweza kufanya kazi hii kwa uzuri wa sura na umbo ajaribu kama hakuchemka.

Source: Mwananchi

TUPE MAONI YAKO

JACKLINE WOLPER AMUENZI KANUMBA KIPEE


MSANII wa filamu nchini Jacklne Wolper amuenzi marehemu Steven Kanumba kivingine kwa kutoa filamu ya 'After Death' ambayo ni mwendelezo wa filamu iliyochezwa na marehemu Steven Kanumba ikiwa ni moja ya kuviendeleza vipaji alivyoacha marehemu Kanumba

Filamu hiyo ambayo pia imezinduliwa siku ya maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja  tangu Kanumba afariki  April 7 katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya kuviendeleza vipaji vya watoto waliocheza na marehemu katika filamu ya Uncle JJ wanaojulikana kwa jina la Patrick na Jenifer

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Wolper alisema kuwa filamu hiyo aliiandaa katika mazingira maalumu kwa ajili ya kumuenzi Kanumba ambaye kila mtanzania anatambua mchango wake kukuza sanaa kiujumla

Alisema kuwa ameamua kumuenzi kwa kutoa filamu hiyo ya muendelezo wa filamu ya Uncle JJ na kucheza na watoto hao ili kuhakikisha anamuenzi kwa vitendo huku akimuombea alale mahali pema peponi

"Filamu ya Uncle JJ ni filamu ambayo yeye mwenye Kanumba alikuwa anaipenda na kuikubali sana hivyo kumuenzi kwa vitendo ni moja ya ya kukamilisha dhamira yake ambayo amejiwekea" alisema Wolper


pro-24
TUPE MAONI YAKO

JACK WOLPER AWAVAA MAPEDESHEE WANAOPENDA KUTUKUZWA

Kama unakerwa na tabia za mapedeshee wapenda sifa kwa kutajwa kwenye nyimbo za muziki wa dansi na kumwaga hela ukumbini, hauko peke yako. Jacqueline Wolper naye humchefua. 



“Napenda kutumia fursa hii leo kuzungumza kitu fulani kidogo tu ambacho nimekiona mimi,” ameandika Wolper kwenye blog yake. 

“Mara nyingi nimekua nikisikia kwenye nyimbo nyingi za wanamuziki wa Tanzania hata wa maeneo mbali mbali kama Jamhuri ya watu wa Congo wakiwataja watu flani flani ambao inaaminika na watu wenye kipato kikubwa kifedha au huwa wanawasaidia kimuziki hata kimaisha wakati mwingine.

Kinachonishangaza kwanini wanapenda kuwatunza kwenye majukwaa tuu? Hao wanaojiita mapedeshee wanaopenda kutajwa kwenye nyimbo za hao wasanii. Nawaomba mapedeshee waende kwenye vituo vya kulea watoto yatima na kutoa misaada ya kifedha na Inshalah Mwenyezi Mungu atawazidishia.”
TUPE MAONI YAKO

PICHA YA JACQUELINE WOLPER AKIWA NUSU UCHI.....

Hatimaye staa wa fi lamu za Kibongo mwenye heshima tele, Jacqueline Massawe Wolper amenaswa ‘laivu’ akiwa amepiga picha chafu inayoonesha sehemu kubwa ya nyeti zake.
 


Kunaswa kwa picha hiyo, kumevunja heshima ya staa huyo aliyekuwa pekee hajapiga picha ya namna hiyo kati ya mastaa wa kike wanaotamba katika tasnia ya fi lamu hapa Bongo.

Wolper alinaswa na mwandishi  wetu katika sherehe ya ‘bethidei’ ya msanii mwenzake iliyofanyika hivi karibuni Ubungo jijini Dar.


Siku za nyuma, staa huyo aliwahi kukataa kupiga picha kama hiyo alipotakiwa kufanya hivyo na mwandishi wetu katika ufukwe mmoja jijini Dar.

Wolper aliapa kamwe hataweza kupiga picha ya namna hiyo katika maisha yake yote

Credit: GPL

TUPE MAONI YAKO

WOLPER AFICHUA SIRI YA UREMBO WAKE




 Msanii wa filamu Tanzania Jackline Wolper hatimaye amefichua siri ya urembo wake kitu kinachomfanya aendelee kuonekana kuwa  mrembo na kubaki na mvuto wake wa asiri

Akizungumza na Pro-24 ,Wolper alijikuta akiweka wazi anachokifanya ili kuendelea kubaki na urembo huo huku akisisitiza kuwa mazoezi ya viungo vya mwili na kutokunywa bia ni siri kubwa ya urembo wake

Wolper hakusita kuweka wazi kuwa yeye ni mtu wa kula mbogamboga,samaki, maziwa na matunda kwa wingi huku akipata muda wa kupumzika ili kujenga mwili wake bila ya kusahau kunywa maji kwa wingi kwani hayo yanamfanya ngozi yake iendelee kuwa yenye mvuto

Wolper alisisitiza kuwa katika maisha yake hutumia kula nyama nyeupe na kuepuka nyama nyekundu ili aendelee kubaki hivyo alivyo na kuepuka kuwa mnene na kutoka kitambi kama baadhi ya wanawake wengine wanavyokuwa


TUPE MAONI YAKO

"NIMEANDAA FILAMU MPYA AMBAYO NITAMSHIRIKISHA LULU MICHAEL"....JACKLINE WOLPER

MSANII wa filamu Tanzania Jackline Wolper ameandaa filamu mpya atakayoshirikiana na  msanii maarufu Elizabeth Michael 'Lulu' itakayokamilika hivi karibuni baada ya msanii huyo kutoka gerezani kwa dhamana

Akizungumza na Maisha Wolpa alisema amepata faraja baada ya taaratibu na sheria kufuatwa na hatimaye Lulu kuweza kupata dhamana hivyo anatarajia kufanya naye kazi ya filamu mpya itakayoanza kurekodiwa baada ya msanii huyo kufika uraiani

Alisema kuwa anatarajia atafanya vizuri katika filamu hiyo kwani tangu awali alikuwa akifanya vizuri katika tasnia hiyo ya uwigizaji kabla ya kupatwa na matatizo

"Nimeshampokea Lulu tangu moyoni mwangu kwani kule alikokuwepo si sehemu nzuri na ukiangalia bado ni mtoto mdogo hivyo inaumiza sana" alisema Wolper

Filamu hiyo ndiyo itakayokuwa ya kwanza kuchezwa na Lulu baada ya kufika Uraiani

Wakati huo huo Rose Ndauka alisema ni wakati wa wasanii kumpokea mwenzao kwani wote ni familia moja na wanahitaji kushirikiana katika kila hali

Alisema kuwa ukiangalia umri wa msanii huyo ni mdogo hivyo ananafasi kubwa bado ya kutengeneza maisha yake na kuangalia wapi amekosea na wapi anapaswa kurekebisha

Naye msanii Single Mtambalike 'Richie Richie' alisema anashukuru kuona sheria imechukua mkondo wake na hatimaye sasa ameweza kuachiwa kwa dhamana hivyo kwa upande wao ni faraja kubwa kwani wote ni familia moja

Alisema anaamini sasa ataweza kujipanga na kufanya kazi vizuri kwani anakipaji na bado wanamuhitaji watanzania kulingana na uwezo mkubwa alionao kwenye tasnia hiyo
TUPE MAONI YAKO

"MWAKA HUU JACK WOLPER HANA BWANA WA KUMCHUNA".....RAFIKI YAKE AVUJISHA SIRI


INAWEZEKANA yakawa ni mazoea......

Msanii wa filamu bongo, Jackline Wolper, ambaye inadaiwa kuwa ndiye anayewafunika mademu wenzake kwenye tasnia hiyo kwa kumiliki mshiko mrefu, inadaiwa kuwa amekuwa akiwaza ndani ya mwaka huu atampataje bwana wa kumuhonga vitu vya kifahari kama bahati ilivyomdondokea msimu uliopita kutoka kijana mtafutaji Dallas.

Kuvuja kwa siri hii kumekuja siku chache  baada ya mwandishi wa dt  kufanya mazungumzo na baadhi ya wapambe wa msanii huyo, ambapo mmoja wao alidai kuwa msanii huyo kwa sasa hana mwanaume anayeweza kumpa vitu ya kifahari kama ilivyokuwa msimu uliopita, hata zile misheshe za kutoka hapa na pale zimepungua kutokana na hilo.

“Rafiki yangu bado hajapata mtu bwana najua ungeona kelele za mjini, saivi yupo tu kama hivi hamna mpya” kilidai chanzo.

Pamoja na ishu hiyo kuvuja Wolper aligoma kuzungumzia ishu hii badala yake alidai kuwa hakuna mtu anayejua siri zake na kama kuna mtu anajua basi abaki na hizo alizonazo.
TUPE MAONI YAKO

JACKLINE WOLPER NA IRENE UWOYA NDANI YA BIFU ZITO


BODIGADI wa mwigizaji kiwango Bongo, Irene Uwoya, aliyetajwa kwa jina moja la Mariam anadaiwa kumshushia kipigo mwigizaji Jacqueline Wolper chanzo kikidaiwa kuwa ni mwendelezo wa bifu lililokuwa limefifia kati ya mafahari hao wa sinema za Kibongo.

Kwa mujibu wa chanzo makini, sheshe hilo lilitokea Desemba 31, mwaka huu  katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar, wakati mastaa mbalimbali walipokuwa wakisherehekea kuupokea Mwaka Mpya wa 2013.


Chanzo hicho makini kiliweka wazi kuwa, wakati shamrashamra za mwaka mpya zikiendelea, ghafla bodigadi huyo wa Uwoya, alimvaa Wolper aliyekuwa anacheza muziki na kuanza kumvuta cheni yake kisha kumshushia kipigo kizito.

“Mariam na Uwoya walikuwa wamekaa pamoja wakipiga kilevi na kustorisha, ghafla tukashangaa mpambe huyo ameinuka na kwenda kumvaa Wolper ambaye alikuwa bize kucheza muziki,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:

“Uwoya atakuwa kamtuma kwa sababu haiwezekani wakae wote halafu dakika chache mbele, ainuke na kwenda kumfanyia fujo mwenzake (Wolper). Hapa kuna kitu.”

Tofauti na ilivyodhaniwa na wengi kwamba bodigadi huyo alitumwa na Uwoya, baada tukio hilo Klabu ya Bongo Movie Unit iliitisha kikao cha dharura ambapo ilidaiwa kuwa Uwoya alikana kuhusika na akamlaani Mariam kwa kitendo hicho cha kumfanyia vurugu Wolper.

 “Wasani wengi walijua Uwoya ndiye aliyetengeneza mchongo mzima lakini kikao kimekataa na kumuona Mariam ndiye mkosaji,” kilisema chanzo hicho.

Baada ya kusikia maelezo ya kikao cha klabu, mwandishi wetu alimtafuta Wolper na kumuuliza juu ya ishu hiyo ambapo alijibu kwa kifupi:

“Siwezi kuzungumza chochote kuhusu hilo, watafuteni viongozi wetu,” alisema Wolper.


Kumbukumbu inaonesha mwaka jana, mastaa hao waliwahi kuwa ndani ya bifu zito ambapo baadaye walipatanishwa na mdau wa burudani maarufu kwa jina la Daudi Kipunguni maeneo ya Mlimani City jijini Dar.
CREDIT:  GPL
TUPE MAONI YAKO

" USTAA WANGU UMETOKANA NA KUUZA SABUNI"........MKASI NA JACK WOLPER


JACK WOLPER
TUPE MAONI YAKO
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger