Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » "SIKUENDA UINGEREZA KUUZA SURA.." IRENE WOYA

"SIKUENDA UINGEREZA KUUZA SURA.." IRENE WOYA

tangazo

MSANII mahiri wa filamu Irene Uwoya, ameamua kuweka wazi kuwa safari yake aliyowahi kuifanya ya nchini Uingereza mwaka jana kwa ajili ya mazungumzo ya kufanya filamu ya kimataifa bado hayajazaa na matunda na hadi sasa wapo kwenye mazungumzo.

Kauli ya msanii huyo ilimfanya mwandishi wetu  amdadisi zaidi, ambapo alisema kuwa kwa sasa kitu wanachokizungumzia ni namna watakavyoandika story ingawa hakutaka kuweka wazi ni story ya namna gani.

Hata hivyo alisema kuwa bado hawajafikia mazungumzo ya kulipwa kiasi gani na lini watafanya lakini anaamini kila kitu kitakuwa safi kwani watu hao wameonesha nia ya kufanya nae kazi.

Pamoja na hayo alishindwa kuwaweka wazi watu hao hata kwa kuwataja majina, kwa madai kuwa kwa sasa siyo wakati wake kwani muda ukifika mashabiki wake watajua anaenda kufanya kazi na kampuni gani.

“Bado tunaendelea na mazungumzo.Sikuenda  huko kuuza  sura .Najua watu wanasubiri kuona ukweli juu ya maneno yangu haya lakini nachotaka kusema ni kwamba ni kweli nilienda kwa ajili ya mazungumzo ila bado mambo hayajakaa sawa,” alisema Uwoya
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger