Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » ULINZI WAIMALISHWA KWA WANAFUNZI WA IFM BAADA YA KASHFA YA UBAKAJI NA KUIBIWA NA VIBAKA

ULINZI WAIMALISHWA KWA WANAFUNZI WA IFM BAADA YA KASHFA YA UBAKAJI NA KUIBIWA NA VIBAKA

tangazo


UONGOZI wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamazi wa Fedha (IFMSO) cha jijini Dar es Salaam, umesema hali ya usalama kwa sasa katika Hosteli za Kigamboni inaridhisha.
Waziri Mkuu wa IFMSO, Daniel Sarungi alisema jana kuwa tangu iundwe timu ya polisi inayoshirikiana na wanafunzi hao hali imekuwa tulivu kwa kipindi cha wiki moja iliyopita. 
Sarungi alisema kuwa hakujatokea uvamizi tena katika hosteli zao, lakini akaongeza kusema kuwa taarifa kamili ya ripoti ya timu hiyo itatolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova.
“Kuna amani sana, misako imefanyika lakini ripoti itatolewa Januari 30 na Kamanda Kova,” alisema Sarungi.
Kauli ya Kiongozi huyo wa wanafunzi haikutofautina na ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Englbert Kiondo, ambaye alisema taarifa inayohusu hali ilivyo itatolewa na Kamanda Kova.

Kwa upande wa wakazi wa Kigamboni, walisema kuwa wameshuhudia polisi wakifanya doria maeneo hayo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma kabla wanafunzi hawajaandamana.
Walisema pia wameona polisi wakiwakamata wahalifu kwenye maeneo hayo kutokana na misako wanayoifanya hali ambayo imeleta utulivu kwenye mji huo.
“Kwa sasa kumetulia inawezekana wanasikilizia (wahalifu), likini ingetakiwa polisi wawakamate wale vinara kwa sababu wanawafahamu” alisema Salum Rashid mkazi wa eneo hilo.
Naye mkazi mwingine anayejishughulisha na biashara ya kioski, alisema kuwa kumekuwa na utulivu kwani hata wanafunzi ambao ndiyo wateja wake wakubwa wanamwambia kuwa wanaweza kuacha vitu wakavikuta salama.
Mwananchi

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger