Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » "MFUMO WA DIGITALI UMENIFANYA NISHINDWE KUIACHIA VIDEO YANGU MPYA.."...KEISHA

"MFUMO WA DIGITALI UMENIFANYA NISHINDWE KUIACHIA VIDEO YANGU MPYA.."...KEISHA

tangazo

Hitmaker wa ‘Usinicheke’, Keisha amesema ameshindwa kuachia video yake mpya kutokana na mfumo wa matangazo ya televisheni wa digitali kuwaacha nje mashabiki wengi wa muziki hasa katika jiji la Dar es Salaam.


Keisha ni miongoni mwa wasanii wengi walioingiwa na moyo mzito wa kuachia video zao kipindi hiki kwa hofu kuwa itatazamwa na watu wachache kwakuwa watu wengi hawana ving’amuzi.

Akiongea na Enews ya EATV, Keisha amesema hali hiyo haijamuathiri yeye tu bali wasanii kibao akiwemo Hemedy Phd ambaye naye anasita kuitoa video yake.

Amesema kulingana na mambo yanavyoenda, anaweza kuiachia hivyo hivyo, ila wasiwasi wakeu mkubwa upo kwa wale wenye uwezo wa chini ambao wanapenda kazi zake.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger