Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » KICHANGA CHATUPWA KATIKA DAMPO LA TAKA....

KICHANGA CHATUPWA KATIKA DAMPO LA TAKA....

tangazo

ZIKIWA zimepita  siku takriban tano toka kukutwa kwa mwili  wa mtoto mchanga katika eneo la Semtema jirani na makazi ya  wanafunzi wa chuo kimoja cha dini mkoani Iringa, simanzi na majonzi zimeendelea kutanda katika Manispaa hiyo baada ya mtoto mwingine wa jinsi ya kike kutupwa katika dampo la taka eneo la Stendi ya M.R mjini Iringa.

Wakizungumzia  matukio hayo ya wanawake wasiofahamika  kufanya vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto wanaowazaa, baadhi ya akina mama wamelitaka jeshi la polisi na jamii nzima kusaidiana kuendesha misako dhidi ya  wanawake  wanaofanya vitendo hivyo vya kikatili.


Sarah Sanga, mkazi wa Miyomboni mjini hapa alisema kuwa  matukio ya wanawake kutoa mimba na kutupa watoto  yameendelea na kuwa ni tishio katika Manispaa ya Iringa.


Bwana Said alishauri wanawake kuwafichua wenzao ambao siku za karibuni walionekana na mimba na ghafla mimba hizo kutoweka kwani  wanaweza kuwa wahusika lakini akawalaumu wanaume kwamba wanaweza kuwa chanzo cha tatizo hilo.


Mkuu  wa Wilaya  ya Iringa, Dk. Leticia Warioba akizungumzia tukio hilo amewataka mabinti na vijana wilayani hapo kuepuka  kupeana  mimba bila kuwa na uhakika wa ndoa.


“Serikali ya wilaya itaendelea kutoa elimu zaidi kwa vijana ili  kupunguza tatizo la watoto  kutupwa katika wilaya ya Iringa,”
alisema 


Jeshi la  Polisi Mkoa wa Iringa, limethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kuahidi  kuendelea na msako mkali  ili kuwakamata  wahusika.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger