tangazo

Papa Emeritus .
Papa Benedikto wa 16 amejiuzulu rasmi leo kama kiongozi wa kanisa katoliki duniani ambapo katika hotuba yake ya mwisho kwa umati wa watu zaidi ya laki moja na nusu waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Benedikto wa 16 ambaye ni mzaliwa wa Ujerumani amezungumzia changamoto zilizolikumba kanisa wakati akiwa kiongozi wake, na kusema kuwa kuna wakati ilionekana kwake kama Mungu amesinzia.
Hata hivyo, ameongeza kuwa mara zote alifahamu kuwa Mungu ndiye nahodha wa meli ya kanisa katolik, na kwamba kamwe asingeiacha meli hiyo izame.
Kesho Siku ya Ijumaa makardinali wataanza mchakato wa kumchagua papa mpya.
Kuanzia sasa Benedikti wa 16 atajulikana kama Papa Emeritus na atahamia katika chumba cha kitawa mjini Vatikani mwezi Aprili.