tangazo

Ronaldo akishangilia moja ya bao lake

Sergio Ramos akiwa mgongioni kwa Ronaldo wakishangilia bao la uongozi

Wachezaji wa Barca chini ya nahodha Carles Puyol wakilalamikia moja ya maamuzi ya refa


Rafael Varane akiifungia Madrid bao la tatu kwa kichwa, akiwazidi kupaa mabeki wa FC Barcelona

Hapa Gerard Pique akimwangusha chini Ronaldo na kusababisha Madrid kupewa penati

Ronaldo kulia akifunga mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kuangushwa chini na Pique

Hapa Ronaldo 'aki-slide' kushangilia bao la pili aliloifungia Madrid

Kocha Jose Mourinho akimkumbatia Rafael Varane baada ya kuifungia Madrid
BARCELONA, Hispania
Beki
Jordi Alba akaifungia bao la kufutia machozi Barca katika dakika ya 89,
lakini halikutosha kuiepushia kichapo hicho, na kujikuta wenyeji hao
wakikubali kufungwa nyumbani mabao matatu na Madrid kwa mara ya kwanza
tangu Machi 2007
MSHAMBULIAJI Cristiano
Ronaldo usiku ya juzi alifunga mara mbili kuipa Real Madrid ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya FC Bracelona, katika mechi ya marudiano ya nusu
fainali ya Kombe la Mfalme ‘King's Cup.’
Pambano
hilo lilipigwa ndani ya dimba la Nou Camp jijini hapa, ambapo kwa
ushindi huo sasa Madrid ilikuwa ikisubiri mshindi wa nusu fainali ya
pili kati ya Atletico Madrid na Sevilla, ili kujua mpinzani wake wa
fainali ya michuano hiyo itakayopigwa Mei.
Ronaldo,
aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika mechi sita
mfululizo za mahasimu hao 'El Clasicos' akiwa ugenini, wakati
alipotikisa nyavu kwa kwa mkwaju wa penati dakika ya 13 baada ya yeye
mwenyewe kuangushwa na Gerard Pique.
Licha ya
bao hilo, Barca iliendelea kumiliki mpira, huku Ronaldo akibaki kuwa mtu
hatari pekee katika kikosi hicho, akifumua na kukosa mashuti kadhaa,
kabla ya kufunga kwa mpira uliorudi ‘rebound’ ya Angel Di Maria dakika
ya 57.
Ronaldo, ambaye amekuwa akilaumiwa kwa
kushindwa kung’ara katika mechi muhimu, hilo likawa bao lake la 12
katika mechi 18 alizoicheza dhidi ya Barca tangu alipojiunga Madrid
mwaka 2009 na ni mara yake ya pili kufunga mara mbili akiwa Nou Camp.
Madrid
ikatia chumvi katika donda la mechi ya awali wakati Raphael Varane,
ambaye aliisawazishia Madrid katika mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao
1-1 kwenye dimba la Santiago Bernabeu, – alipounganisha kona nyavuni
dakika ya 68 kuipa Madrid bao la tatu.
Beki
Jordi Alba akaifungia bao la kufutia machozi Barca katika dakika ya 89,
lakini halikutosha kuiepushia kichapo hicho, na kujikuta wenyeji hao
wakikubali kufungwa nyumbani mabao matatu na Madrid kwa mara ya kwanza
tangu sare ya 3-3 Machi 2007.
SuperSport.com