tangazo
Kura
zikihesabiwa kwenye kituo kilichopo Viwanja vya Kibera Social, jijini
Nairobi baada ya wananchi wa Kenya kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa
nchi hiyo jana. Picha na AFP
------------
Matokeo
ya awali ya uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha kuwa Uhuru Kenyatta,
mtoto wa Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta anaongoza, huku
akifuatiwa kwa karibu na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Raila
Odinga.
Kama
alivyo Uhuru, Raila pia ni mtoto wa mmoja wa waasisi wa taifa la Kenya,
ambaye alikuwa Makamu wa Mzee Kenyatta, Jaramong Oginga Odinga.
Waliokufa wafikia 22
Wapema
watu 22 wakiwamo askari polisi tisa waliripotiwa kuuwawa baada ya
kuvamiwa na kikundi cha watu zaidi ya 200 huko Mombasa na Kilifi saa
chache kabla ya Wakenya kuanza kupiga kura jana.
Saa
chache kabla ya uchaguzi huo, askari polisi tisa waliuawa katika
mashambulizi yaliyotokea kwenye miji ya Mombasa, Kilifi na Kwale na
kuacha wavamizi wapatao 10 na raia wa kawaida watatu pia wakifariki.
Baada
ya vifo hivyo, serikali ilipeleka vikosi vya askari kutoka Mariakani
Barracks kwenda kutuliza ghasia hizo wakati kundi lingine la askari
lilitoka Nyali Barracks kwa ajili ya kuweka doria katika miji ya Mombasa
na North Coast.
Taarifa
zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa kwenye mji wa Mombasa askari
polisi wanne waliuawa na watu zaidi ya 100 waliovamia kituo cha kura cha
Miritini.
Polisi pia ilithibitisha kuuawa kwa watu saba katika mapigano hayo huku na wengine kadhaa kutiwa nguvuni.
Wavamizi
wengine waliuawa katika miji ya Kisauni na Kilifi huku polisi wanne
wakiuawa Chumani na mmoja huko Chonyi huku watu watatu wakiuawa kwa
kupigwa risasi.
Mwanachi