Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » PENZI LA FACEBOOK LASABABISHA BIBI WA MIAKA 67 AUAWE NA MPENZI WAKE WA MIAKA 28 AMBAYE WALIKUWA HAWAJUANI

PENZI LA FACEBOOK LASABABISHA BIBI WA MIAKA 67 AUAWE NA MPENZI WAKE WA MIAKA 28 AMBAYE WALIKUWA HAWAJUANI

tangazo

Polisi wa Afrika Kusini bado wanaendelea kuchunguza tukio la kutisha linalodaiwa kufanywa na kijana wa Kinigeria mwenye umri wa miaka 28 ambae anatuhumiwa kumuua bibi wa kizungu mwenye umri wa miaka 67 huko Johannesburg.

Bibi kizee Jette Jacobs ambae ni raia wa Australia alisafiri mpaka Johannesburg kwa lengo la kufunga ndoa na mwanaume anayempenda lakini siku mbili baada ya kukutana na mwanaume huyo, bibi huyo amekutwa amefariki kwenye mazingira ya kutatanisha kwenye jiji hilo lililo kwenye list ya majiji hatari kwa uhalifu duniani.

 
Jette alipokwenda Johannesburg lengo lake lilikua ni kukutana kwa mara ya kwanza na mwanaume ambae wamekua wakiwasiliana kupitia mtandao wa kijamii ambao hukutanisha watu wenye hitaji la kupata mpenzi/mke/mume ambapo aliingia kwenye mapenzi na Jesse Orowo Omokoh asiemjua miaka mitatu iliyopita.
 
Mwili wa bibi huyu mwenye watoto sita ulikutwa kwenye guest house miezi miwili baada ya kuwasili Afrika Kusini ambapo kwa muda waliofahamiana online, Jette alikua ameshatuma kiasi cha dola za Kimarekani laki mbili kwa Omokoh na mwanaume mwingine aitwae Isaac.
 
Pamoja na kupewa onyo na familia yake, Jette hakusikia chochote bali alitaka kwenda South Africa toka november 2012 ili akafunge ndoa na huyu mwanaume wa Kinigeria, kwenye guest house mwili wake ulipokutwa kuna baadhi ya vitu alivyokuwa navyo havijaonekana kama vile mikufu na pesa.
 
Binti wa mwisho wa bibi huyu amesema mwanaume huyu wa Nigeria alitaka kuhamia Australia ili akaishi na Bibi huyu lakini bibi aligoma na kumwambia anataka kwenda kuishi nae Nigeria.

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger