Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » IRENE UWOYA AJIPANGA KUAJIRI WAIGIZAJI 30 TOKA MIKOA YA DODOMA NA MOROGORO KWA AJILI YA MOVIE MPYA

IRENE UWOYA AJIPANGA KUAJIRI WAIGIZAJI 30 TOKA MIKOA YA DODOMA NA MOROGORO KWA AJILI YA MOVIE MPYA

tangazo

Mugizaji wa filamu nchini Irene Uwoya aka Mama Krish, amewakata wakazi wa Morogoro na Dodoma wenye vipaji vya kuigiza kujiandaa kwanini hivi karibuni anaandaa mchakato wakutafuta waigizaji zaidi ya thelathini (30) kwa ajili ya kuigiza naye movie yake mpya itakayotoka mwishoni mwa mwezi wa sita au mwanzoni wa mwezi wa saba.
 


Uwoya amesema kutakuwa na usaili kwa ajili ya kuwapata waigizaji hao na ametaka vikundi vya uigizaji kujiandaa na kujipanga kwani movie hiyo itakuwa ya kwanza na ya aina yake katika historia ya movie za kibongo.

Irene Uwoya ameuambia mtandao wa Bongo Movies, “Watu wamezoea kumuona Irene akigiza ndani ya nyumba nzuri na magari mazuri kila siku, hawajui kama Irene huyu huyu anaweza kufanya movie kama mtu wa kijijini sana asiyejua hata matumizi ya simu ni nini. Nataka kufanya kitu cha tofauti kabisa mpaka watu washangae kama ni mimi kweli, hii movie itakuwa ya kwanza Tanzania.”

Katika movie hiyo mpya, Uwoya amesema atashirikisha vipaji vipya tu ambavyo havijawahi kuoneka kwani anaamini bado kuna vipaji vikubwa vimejificha hasa mikoani na anataka kuwapa nafasi ili waweze kuonesha uwezo wao ndani ya tasnia hii ya Bongo Movies.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger