tangazo
Inaonekana tabia ya wasanii wakubwa kufawanyia dhuluma wasanii wachanga inazidi kushamiri everyday.
Habari za uhakika zilizotufikia ni kwamba kundi la muziki la akina dada la Scorpion Girls linaloundwa na Miss Ruvuma 2000, Rashida Wanjara, Bella na Jini Kabula wamemfanyia utapeli upcoming singer and songwriter Soud Salim aka Esmyzer.
“Nilikutana na Scorpion Girls mwaka jana na wakaniomba niwaandikie wimbo, tukakubaliana niwaandikie wimbo then watanilipia studio na mie nirekodi. Nikawaandikia their debut single ‘Watuache’.
Lakini cha ajabu baada ya single yao kutoka nilipoenda studio pale wakaniambia hakuna booking niliyofanyiwa na Scorpion Girls.
Mie nikamuachia mungu, lakini haikuwa muda wakaja tena safari wakiwa na meneja wao Tuddy, wakaniambia niwaandikie tena mie nikakubali kwa sababu ya Tuddy lakini safari hii nilitaka wanilipe fedha.
Tukakubaliana baada ya wiki watakuwa wameshalipa. Siku hiyo niliyokuwa naawandikia ngoma studio pale kwa Tuddy nilikaa nao mpaka usiku sana ndio tukamaliza.
Wakati narudi nyumbani wakanikodishia pikipiki ambayo nilipata nayo ajali bahati nzuri sikuumia sana nikajikokota mpaka home, and to make it worse nilipofika home nikakuta mlango wa ghetto umevunjwa na nimeibiwa karibia vitu vyangu vyote vya ndani.
Nilijaribu kuomba japo msaada kidogo kutoka kwao lakini hakuna nilichoambulia, mpaka sasa hakuna malipo waliyonipatia,” alisema Esmyzer.
baabkubwa