tangazo
MWANAMITINDO
nyota nchini, Joketi Mwegelo, anatarajiwa kunogesha uzinduzi wa kampeni
ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kike,
unaotarajiwa kufanyika keshokutwa, ambapo shughuli mbalimbali na mada
zitatolewa.
Joketi,
ambaye anawika katika tasnia mbalimbali nchini ikiwemo urembo,
mitindo, muziki na filamu, atashiriki kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo
ijulikanayo kama Okoa Mtoto wa Kike Tanzania utakaofanyika katika Kata
ya Nyamongo wilayani Tarime, Mara.
Taarifa
ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyumbani Kwanza Media Group iliyoandaa
kampeni hiyo, Mossy Magere, imesema kuwa maandalizi yote muhimu
yamekamilika na Joketi atawasili wilayani Tarime kesho tayari kwa
kushiriki na atatoa mada ya masuala ya ujasiriamali kwa washiriki wa
tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa.
Mossy
alisema kuwa mbali na Joketi, wasanii mbalimbali watashiriki kutoa
burudani wakiwemo wasanii nyota wa bongo fleva na wale wa asili
wanaotamba mkoani Mara.
'Maandalizi
yote ya msingi yamekamilika na kinachosubiriwa ni muda wa uzinduzi
ufike, Joketi anatarajiwa kuwasili hapa kesho tayari kwa kushiriki nasi.
Atapata fursa ya kutoa mafunzo na mbinu
za kimaisha kwa washiriki ambao wengi ni wanafunzi wa shule mbalimbali wilayani hapa,' alisema Mossy.
Kampeni
hiyo ambayo itadumu kwa kipindi cha miezi sita, itazinduliwa rasmi
keshokutwa na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, ambaye
ameshirikishwa kwa karibu na Kampuni ya Nyumbani Kwanza.
Alisema
mchakato wa uundwaji wa klabu za wapinga unyanyasaji katika shule
mbalimbali za sekondari wilayani Tarime ambapo kampeni hiyo inaanzia
umekamilika na wanafunzi wamevutiwa na kujiunga kwa wingi kwenye klabu
hizo ambazo zitakuwa kichocheo cha kuendeleza kampeni hiyo.
Mossy
aliongeza kuwa, uundwaji wa klabu hizo unalenga kukiwezesha kizazi cha
sasa na kijacho kuwa mstari wa mbele kukataa vitendo vya unyanyasaji.
“Kila
jambo jema huanzia ngazi za chini, kwa sasa tunaendelea kuunda klabu za
wapinga unyanyasaji ambazo zitakuwa zikipewa mafunzo na mbinu
mbalimbali ili kuwajenga kufahamu madhara wakiwa wangali wadogo
shuleni.