Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » KIONGOZI MKUU WA AL-QAEDA AUWAWA

KIONGOZI MKUU WA AL-QAEDA AUWAWA

tangazo


Kiongozi mkuu wa kundi la al-Qaeda ameuawa nchini Mali. Taarifa hizi zimethibitishwa na Rais wa Chad, Idriss Deby Alisema kuwa majeshi ya nchi yalimuua Abdelhamid Abou Zeid, wakati wa makabiliano yaliyotokea katika eneo la vijijini nchini Mali. Anasemekana kuwa wa pili kwa ngazi ya uongozi katika kundi hilo ambalo linapigana na majeshi ya kigeni nchini Mali.

Raia huyo wa Algeria anatuhumiwa kwa mauaji ya mateka wawili kutoka nchi za magharibi Edwin Dyer raia muingereza mwaka 2009 Michel Germaneau raia wa ufaransa mwaka uliofuata. Mwandishi wa BBC Thomas Fessy anasema kuwa ikiwa wataweza kuthibitisha kifo hicho, maswali bila shaka yataibuka kuhusu mateka wa Ufaransa wanaoaminika kuwa walikuwa mikononi mwa Abou Zeid. 

 Mwezi Januari, Ufaransa ilituma wanajeshi 3,500, Kaskazini mwa Mali, kwa lengo la kuwaondoa wanamgambo wa kiisilamu waliokuwa wameteka sehemu ya jangwa la Sahara.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger