Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » "NIMECHOKA KULIZWA NA KERO ZA WAANDISHI WA HABARI".....MAMA KANUMBA

"NIMECHOKA KULIZWA NA KERO ZA WAANDISHI WA HABARI".....MAMA KANUMBA

tangazo

Mama yake mzazi na marehemu Steven Kanumba amesema maswali anayoulizwa kila mara na waandishi wa habari hasa za udaku humfanya asipitishe siku mbili bila kulia kutokana na kumkumbuka mwanae kipenzi.


Akiongea na kipindi cha The Avenue cha TBC 1, mama huyo ambaye hivi karibuni amejiingiza kwenye uigizaji wa filamu pia amesema mara nyingi anapofuatwa na waandishi wa habari kumuuliza maswali kuhusiana na mwanae hubaki akilia na waandishi wa habari huishia kuandika habari za uongo tofauti na alivyoongea.

“Kupoteza mtoto wa miaka 28 sio mchezo, inauma,” alisema Mama Kanumba.

Aliongeza kuwa hawezi kuangalia filamu za mwanae kwakuwa humfanya ajisikie vibaya japo nguo zake bado zipo na huziona kila siku.

TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger