Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » » MATOKEO YA MWISHO YA UCHAGUZI NCHINI KENYA KUTANGAZWA HIVI PUNDE

MATOKEO YA MWISHO YA UCHAGUZI NCHINI KENYA KUTANGAZWA HIVI PUNDE

tangazo

A man passes by posters of presidential candidates Uhuru Kenyatta and Prime Minister Raila Odinga in Nairobi, March 8, 2013.

Ikiwa imebaki saa chache kabla ya kutangazwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais Kenya, bado haijulikani ikiwa Uhuru Kenyatta ataweza kupata asilimia 50 na kura moja kunyakua ushindi katika duru ya kanza.

Wakuu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC walisema mchana wa Ijuma kwamba ingawa matokeo yanatolewa pole pole lakini wanauhakika Wakenya watapata matokeo rasmi usiku wa Ijuma kama walivyoahidi hiyo jana.


Wakiwa wameshatangaza matokeo ya wilaya 252 za uchaguzi kati ya 291, Uhuru Kenyatta anaongoza akiwa na kura 5, 418, 291 ikiwa sawa na asili mia 49.72, huku mpinzani wake wa karibu Raila Odonga ana kura 4, 689,997 sawa na asili mia 43.

 
wagombea wngine wa kiti cha rais wameanza kukubali kushindwa, Peter Kenneth aliwashukuru wafuasi wake walomunga mkono na kusema yuko tayari kufanya kazi na mtu yeyoter atakae shinda.


Musalia Mudavadi, mgombea kiti cha rais wa mungano wa AMANi alyetarajiwa kuwaletewa changamoto kubwa Uhuru na Raila alitangaza mapema Ijumaa kwamba  kutokana na hesabu ni wazi mashindano ni kati ya mafahali wawili na anasubiri matokeo ya mwisho.
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger