Ungana nasi kwa kuandika email yako hapa ili upate habari mpya kupitia email yako bila usumbufu:


Home » , » MATUMAINI AIANGUKIA SERIKALI IMSAIDIE MATIBABU YA INI NA FIGO

MATUMAINI AIANGUKIA SERIKALI IMSAIDIE MATIBABU YA INI NA FIGO

tangazo


KOMEDIANI maarufu Bongo, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ ameiomba serikali imsaidie kupata matibabu ili aweze kupona maradhi ya figo na ini yanayomkabili.

Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam alisema: “Hali yangu bado si nzuri ingawa natumia dawa lakini sijapata tiba sawasawa. Sina fedha na familia yangu kwa sasa imeishiwa kwa sababu magonjwa yanayonisumbua ni makubwa na yanahitaji fedha nyingi.

“Naiomba serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo isikie kilio changu. Hali yangu si nzuri, nahitaji msaada ili kuokoa maisha yangu. Nina imani  nikipata tiba kamili nitapona na kurejea tena jukwaani.”
TUPE MAONI YAKO
KAMA UMEGUSWA NA HUDUMA ZETU, TUNAOMBA UUNGANE NASI KATIKA PAGE YETU YA FACEBOOK HAPO CHINI. BOFYA "LIKE" KAMA BADO HUJA LIKE PAGE YETU.
KUMBUKA KU LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK
 
Support : mpekuzi | John mpekuzi | Wataalam
Copyright © 2009. DOMO LANGU - All Rights Reserved
Template designed by mpekuzi
Proudly powered by Blogger